Main Title

source :
Jumatatu

22 Oktoba 2012

16:19:00
358791

Elimu ya Tiba na historia yake sehemu ya pili Na:Mketo Matenga

Maisha ya Ibn siina(Avecina)

Makala iliopita tulieleza kwa ufupi Historia ya Tiba katika uisilamu, na kuashiria baadhi ya madaktari wa kiislamu, ambapo miungoni mwao alikuwa daktari mashuhuri Ibun Siina(Avecina). Ama katika makala hii nitazungumzia maisha yake kwa ufipi na kugusia baadhi ya nukta muhimu za Elimu ya Tiba katika Qur'an na mtazamo wake kunako masuala ya Tiba na taaluma mbalimbali za Tajiruba. Kuwa pamoja name ndugu msomaji katika kuangalia misingi ya kiislamu kunako Elimu za Tajiruba.

Avicena alizaliwa mwaka 370 A.H Sehemu ya Balakh ambayo ni Iaran ya zamani na hivi sasa ni miungoni mwa sehemu ya nchi ya Afghanistani, baba yake alikuwa  mwana siasa na nimiungoni mwa wanazuoni maarufu, Avicinna alilelewa katika mazingira ya kiimani sambamba na dini ya kiisilamu, ambapo katika miaka kumi ya awali alijifunza Qur’an na elimu za Lugha, pia alijifunza  Elimu za kiakili na hesabu kwa bwana Mahmudi  Masaha na kusoma Elimu ya Mantiki  kwa bwana Natly, pia kujifunza alimu za Sheria na Kifiqihi kwa bwana Ismail  Zahid.
Imeelezwa kuwa Avicenna alikipitia kitabu cha Arustrit mara arubaini, pia alikuwa anachunga sana masuala ya Imani, Dini na Sheria zake, nae alikuwa mtu wa ibada saada na mwenye jitahida katika kutafsiri  Qur’an na kuihifadhi na kujifunza Elimu ya Hadithi. Alianza kujifunza Utabibu  na Udaktari akiwa na umri wa miaka 16 nae alikuwa akisema: katika muda mchache nilipokuwa ni kujifunza Elimu ya Tiba nilipata umahiri na uwezo mkubwa wa Elimu hiyo, na nikapata umaarufu mkubwa na kufahamika sana katika kutibu wagonjwa.
Avicenna aliendelea na harakati zake hizo mpaka mnamo mwaka 428 A.H akafariki na kuitika wito wa molawake. Ama Kuhusiana na mahala alipo fia kunatafauti baina ya wana Historia kama ifwatavyo: baadhi yao wanasema alifia hamadani na wengine husema amefia Isfahani, vyovyote vile iwavyo ibun sina amezikwa hamadani na kaburi lake  linapatikana hapo.
Kuathiriwa kwake na mafunzo ya Kiislamu 
Kama nilivyo sema hapo mwanzo kuwa Avecenna alijitahidi kutafsiri Qur’ani na kujifunza Elimu ya Hadithi, hivyo basi vitu hivi vilikuwa vinamchango mkubwa katika Elimu yake  na hapa nitaashiria nukta muhimu zifuatazo:
1-Lengo la kuteremshwa  Qur’an ni kumlea na kumuongoza Mwanadamu katika masuala ya kiroho na kumfikisha Mwanadamu huyu katika saada, ukamilifu na uzima wa milele, na hapa jambo la kuzingatiwa ni kwamba ijapokua  Qur’an imeelezea kwa mapana zaidi saada ya mwanadamu lakini pia haikuacha kuashiria  masuala ya kisayansi na elimu za Tajiruba, na kuashiria kwake masuala hayo hakumaanishi kwamba  Qur’an imegeuka kuwa ni kitabu cha sayansi. kwani Elimu ya Sayansi na Tajiruba zinaweza kufikiwa na akili ya Mwanadamu pekee kwaminajili hiyo hakuna maana kusema kuwa  Qur`an  nikitabu cha Elimu za Tajiruba. ama kuashiria kwa  Qur’an kunako masuala hayo ni kama ifuatavyo:
A-Kumshajiisha Mwanadamu katika kumjua Mola Muumba wake
B-Kumfanya Mwanadamu awe mchunguzi katika masuala ya Elimu ya Tajiruba
C-Kuwashajiisha Waisilamu na wanadamu katika kutafuta Elimu katika Nyanja tafauti .kwaminajili hiyo  Qur’an sikitabu cha Tiba mpaka Wanadamu watarajie Elimu ya Tiba kutoka kwenye Qur’an la hasha sivyo hivyo kwani Elimuhizi zinaweza fikiwa kwa akili aliopewa mwanadamu. 
Ama kugusia kwake Qur’ran katika baadhi ya masuala ya kitiba na elimu zingine za Tajiruba kamavile:utungaji wa ujauzito, alam za mikono, uponyaji wa asali,  Afya ya mwili na usalama wake, na… yote hayo ni kwaajili ya kumfanya Mwanadamu atafakari  katika alama za kuwepo Molawake muumba na kuamsha hisia za mwanadamu huyu kunako utafiti katika masuala ya sayansi na Tajiruba.
2-Hakuna dini au kundi lolote la kiimani lilioipa kipaumbele elimu na kusisitiza kunako elimu kama ilivyo sisitiza dini ya kiisilamu, kiasi kwamba daraja ya msomi na mwananzuoni mwenye imani nitafauti na muumini asiekuwa na elimu, na Mwenyezi mungu anasema katika Qur’an  surat mujadalah aya 11 akisema :
یرفع الله الذین آمنوا والذین اوتواالعلم درجات
Mwenyezi mungu atawanyanyua wale walioamini miungoni mwenu, na wenye elimu atawapa daraja la juu.
na neno(elimu)katika Qur’an limekaririwa mara 80 pia neno(wenye utambuzi) na (wenye akili) limekaririwa zaidi ya mara 10 na aya zinginezo nyigi zikiwataka wanadamu wawe wenyekutafakari na kuzingatia na…
Haya yote yanaashiria  kuwa uisilamu umezingatia  zaidi na kuhimiza suala la Elimu na kutumia akili. pia upande wa hadithi za mtukufu mtume(s.a.w) nazo zimehimiza suala la kutafuta Elimu na kutafakari kama alivyo sema mtukufu mtume(s.a.W.w):فکرة ساعة خیر من عبادة سنة
Saa moja katika hali ya kutafakari nibora kuliko ibada ya mwaka mmoja .
Pia anasema mtukufu Mtume(s.a.w.w): kuhudhuria katika kikao cha mwanazuoni ni bora zaidi kuliko kusindikiza majeneza Elfu moja ya waumini, kuwatembelea wagonjwa  elfu moja waumini ,… kufunga siku elfu moja...kwani mwafahamu kuwamba Mungu huabudiwa  kwa Elimu.
Hivyo basi Uisilamu umesisitiza vitu viwili katika jamii ya kibinadamu navyo ni: mwanazuoni, Hakimu, na Tabibu.
Kama alivyosema Imam Swadiq(a.s)kila mji na mkoa wahitaji vitu vitatu :mwanazuoni ,hakimu wa sheria na tabibu au daktari.
Semi hizi na wito huu wa uisilamu ndio uliomfanya ibun siina abobee katika Nyanja tofauti kwani yeye alikuwa mtaalamu wa elimu tafauti, falsafa, Erfani, Hesabu, Utabibu, na…nae ndie pekee  alieikosoa tiba ya Jalinusi katika kitabu alichokiandika Ibun Siina kiitwacho(Qaanun)
                                                          ***
Hivyo aveccina alizaliwa mwaka 370 A.H katika sehemu ya Balakh na kulelewa katika mazingira ya kiisilamu hatimae kujifunza Elimu za dini na baadae kujifunza Elimu za Sayansi na Tajiruba na kupata umarufu mkubwa duniani hapo zamani hadi sasa. na amefariki mwaka 428 A.H (Mungu amuweke  mahala pema peponi).