Kipindi
-
Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Washia Lebanon: Iran Inaingia Katika Kipindi Kipya cha Nguvu
Sheikh Ali Al-Khatib amesema kuwa baada ya kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, Iran imeingia katika hatua mpya ya nguvu, akisisitiza kuwa misingi ya fikra, dini na maadili ya uongozi wake imejikita kwa kina miongoni mwa Wairani, Waislamu na watu huru duniani.
-
Msemaji wa Jeshi la Iran: Tunaimarisha Uwezo wa Kijeshi Wakati wa Usitishaji Mapigano na Tutajibu Kwa Nguvu Shambulio Lolote
Msemaji wa Jeshi la Iran amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vinatumia kipindi cha usitishaji mapigano kuimarisha uwezo wake wa kivita, akisisitiza kwamba Iran itajibu kwa uthabiti dhidi ya kosa lolote litakalofanywa na adui. Pia alieleza kuwa mzozo kati ya Iran na Israel ni wa kimkakati na wa kuamua mustakabali wa pande hizo mbili.
-
Marekani Yatoa Leseni ya Muda Kuruhusu Mauzo ya Mafuta ya Iran Hadi Agosti 2026
Wizara ya Hazina ya Marekani imetangaza kutoa leseni inayoruhusu Iran kuuza mafuta ghafi, bidhaa za petrokemikali na bidhaa zake za mafuta hadi tarehe 21 Agosti 2026.
-
Maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Imam Mahdi (AS): Vijana Wakumbushwa Wajibu wa Kuijenga Jamii ya Uadilifu katika Kipindi cha Ghaiba
Katika mnasaba wa maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Imam Mahdi (AS), Waislamu wa Shia na Sunni walikusanyika kujadili kuhusu Mwokozi wa Ulimwengu na wajibu wa Waumini katika kipindi cha Ghaiba. Khatibu Sheikh Suleimani Abdully aliwakumbusha vijana juu ya umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu, kushukuru neema Zake na kujenga tabia njema ili kuandaa jamii yenye utu, uadilifu na iliyoepukana na dhulma na ufisadi.
-
Sheikh Ahmad Haji Atoa Mafunzo Muhimu ya Kujenga Utu na Kukemea Dhulma katika Jamii | "Dhulma huondoa Baraka na Kuleta Majuto"
"Unaweza kumdhulumu mtu na ukalala usingizi mzito, lakini yule uliyemdhulumu halali kamwe. Anakumbuka dhulma yako kila siku na humlalamikia Mwenyezi Mungu dhidi yako. Na ikumbukwe kuwa macho ya Mwenyezi Mungu hayalali,” amesema Sheikh Ahmad Haji, akisisitiza hatari ya dua ya aliyedhulumiwa.