Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Washia nchini Lebanon, Sheikh Ali Al-Khatib, amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeingia katika mwanzo wa kipindi kipya cha nguvu kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Akizungumza katika hafla ya kumbukumbu ya kiongozi huyo, iliyohudhuriwa na wanazuoni mbalimbali wa Kiislamu, Sheikh Al-Khatib alisema Iran kwa sasa inaandika mwanzo wa enzi mpya katika mapambano dhidi ya mataifa ya Magharibi na changamoto zinazotokana na sera zao ambazo, kwa mujibu wake, zimejengwa juu ya ukosefu wa maadili na unafiki.
Aidha, aliikosoa Marekani na viongozi wake, akidai kuwa hutegemea nguvu na mabavu kama nyenzo ya kuendeleza ushawishi wao duniani.
Katika hitimisho la hotuba yake, Sheikh Al-Khatib alisisitiza kuwa misingi ya fikra, dini na maadili ya uongozi wa Iran imeota mizizi ndani ya mioyo ya wananchi wa Iran, mataifa ya Kiarabu, ulimwengu wa Kiislamu na watu wote wanaopigania uhuru duniani.
Maoni yako