Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya anga mashariki mwa Khan Yunis na kuua na kuwajeruhi makumi ya raia. Vikosi vya uokoaji viliopoa miili ya mashahidi na kuwahamisha waliojeruhiwa, huku hospitali zikithibitisha vifo 28, wakiwemo watoto 17.
Mkuu wa Taasisi ya Kuhifadhi na Kueneza Thamani za Ulinzi Mtakatifu na Mapambano ametoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kifo cha Kamanda wa IRGC, Brigedia Sardar Alireza Afshar.