Bibi Zahra (a.s) ni kielelezo cha Mwanamke kamili katika Uislamu - mfano wa ucha Mungu, hekima, upendo wa kifamilia, ushujaa wa kijamii na mapambano ya kiroho.
Maisha yake ni dira ya kudumu kwa wanawake na wanaume wote wanaotaka kufikia ukamilifu wa kibinadamu katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Sheikh Hemed Jalala alisisitiza umuhimu wa malezi bora ya watoto kwa kufuata misingi thabiti ya Kiislamu. Alibainisha kuwa familia ni msingi wa jamii, na hivyo malezi ya mtoto yanapaswa kuakisi maadili na mafundisho ya dini.