Mbele
-
Mchambuzi: “Heiba ya Marekani Yaporomoka Mbele ya Muqawama; Ushindi Wake Ni kwa Serikali Tegemezi Pekee”
Dkt. Hassan al-Rassabi: “Marekani haijashinda dhidi ya mataifa ya Muqawama, bali imefanikiwa tu kwa serikali tegemezi; heba ya Washington imeporomoka kimkakati.”
-
Rais Pezeshkian: Vitisho vya Kulenga Miundombinu Vinadhihirisha Udhaifu Dhidi ya Uamuzi wa Taifa
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema kuwa vitisho vya kushambulia miundombinu muhimu ya nchi hiyo vinaonyesha udhaifu wa wapinzani mbele ya uamuzi na mshikamano wa wananchi wa Iran.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Vikosi vya Iran Havitasita Kuilinda Nchi na Kujibu Uchokozi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, amesema matukio ya usiku uliopita yameonyesha wazi kuwa vikosi vya ulinzi vya Iran viko tayari kuitetea nchi wakati wowote, huku akiilaumu Marekani kwa kudhoofisha mchakato wa kidiplomasia kupitia ujumbe unaokinzana na ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji vita.
-
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi: Iran Ipo Mstari wa Mbele wa Mhimili wa Muqawama
Hujjatul-Islam Mohammad Taqi Vakilpour amesema Iran ipo mstari wa mbele wa mhimili wa muqawama pamoja na Lebanon, Palestina na Yemen, huku akisisitiza umuhimu wa umoja wa kitaifa, kuimarisha mfumo wa Kiislamu na kukabiliana na juhudi za maadui za kueneza migawanyiko ndani ya jamii.
-
Msemaji wa Jeshi la Iran: Hatuwezi Kuvumilia Kuendelea kwa Uhalifu Dhidi ya Lebanon
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran, Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, ameonya kuwa Iran haitakaa kimya mbele ya kuendelea kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon, akilaani mauaji ya raia na ukimya wa baadhi ya mataifa ya Magharibi.
-
Vikosi vya Urusi Vadai Kuuteka Kikamilifu Mji wa Kupyansk Huko Ukraine - Ukraine Yakanusha!
Kwa sasa, hali ya Kupyansk inaelezwa kuwa bado ni ya mvutano mkubwa, huku mashambulizi ya mabomu, droni na silaha nzito yakiendelea kuripotiwa katika maeneo ya karibu.