Moshi
-
Tanzania -Kigoma | Sheikh Hussein Moshi Abdallah Aendelea Kutoa Mafunzo ya Dini Katika Taasisi ya Imam Sajjad (as) Mkoani Kigoma
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Imam Sajjad (as), Sheikh Hussein Moshi Abdallah, anaendelea kutoa elimu ya dini kupitia darsa zake za kila siku zinazofanyika katika taasisi hiyo, iliyopo Kasuku, mkoani Kigoma, Tanzania, kwa lengo la kueneza mafundisho ya Kiislamu kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu na mafundisho ya Ahlul-Bayt (as).
-
Dkt. Ali Taqavi Atembelea Vituo vya Elimu ya Dini na Ufundi Stadi Mjini Moshi, Asisitiza Maadili na Malezi ya Kiislamu
Rais wa Uwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s.a.w.w.) nchini Tanzania, Hujjatul Islam wal-Muslimin Dkt. Ali Taqavi, amefanya ziara ya kida‘wa katika vituo mbalimbali vya elimu ya dini na ufundi stadi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambapo amekutana na wanafunzi na waumini, akisisitiza umuhimu wa maadili mema, kauli njema na mshikamano wa kijamii katika mafundisho ya Uislamu.
-
Maulid ya Mtume Muhammad (saw) Yaadhimishwa kwa Pamoja na Waislamu wa Madhehebu Mbalimbali Mjini Moshi
Sherehe kubwa ya Maulid ya Mtume Muhammad (saw) imefanyika katika Madrasat Ummul-Banin (sa), mjini Moshi, Tanzania, kwa kushirikisha Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni. Hafla hiyo imekuwa jukwaa la kuimarisha upendo, undugu na umoja wa Kiislamu, pamoja na kueneza mafundisho ya Mtume (saw) na Ahlul-Bayt (as).
-
Darsa za Kielimu na Maarifa | Mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s) Yaendelea kuwaangazia Waumini Kila Alhamisi Mjini Moshi +Picha
Kupitia mihadhara hii, waumini hupata fursa ya kujifunza misingi ya itikadi, maadili ya Kiislamu, na mwongozo wa maisha unaojengwa juu ya haki, uadilifu na kumcha Mwenyezi Mungu.