Naeem

  • Sheikh Naeem Qassem: Iran Daima Iko Kando ya Muqawama / Mmekuwa Mfano kwa Dunia Nzima

    Tukio la “Iran Moyo Mmoja”:

    Sheikh Naeem Qassem: Iran Daima Iko Kando ya Muqawama / Mmekuwa Mfano kwa Dunia Nzima

    Sheikh Qassem pia aliipongeza Iran ya Kiislamu kwa kusimama kwake kwa ushujaa mkubwa dhidi ya uvamizi wa Marekani na Israel kwa kipindi cha siku kumi na mbili, akisema: “Alhamdulillah, mmeonyesha mfano kwa dunia nzima jinsi ya kupambana na uvamizi, kusimama imara, na kufikia mafanikio makubwa kwa baraka za uongozi wa Imam Khamenei (h.a), umoja wa watu na uaminifu wa wanajeshi wenu shupavu. Ushindi huu utaandikwa katika historia.” Akaongeza kwa kusisitiza: “Tunajua Iran inalipa gharama kubwa kwa kusimama upande wa haki, upande wa muqawama, upande wa Palestina, na upande wa mataifa yote yanayohitaji msaada. Lakini hii ndiyo Iran — mfano wa kujitolea, utukufu na uadilifu — ambayo haidai chochote kwa kusimama na wanyonge. Iran hii imesimama kwa ajili ya utukufu wa ubinadamu.” Sheikh Qassem alizungumzia pia vikwazo vipya dhidi ya Iran, akisema: “Leo tena wameiwekea Iran vikwazo vipya. Je, vikwazo hivi viliwahi kuacha kuwepo? Tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu miaka 46 iliyopita, Iran imeendelea kuwa chini ya vikwazo, lakini kila siku taifa hili limeendelea kung’aa zaidi na kuthibitisha kuwa ni taifa la ukweli na la mapambano.”

  • Uvamizi wa Wazayuni Dhidi ya Qatar Ni Sehemu ya Mradi wa "Israeli Kubwa"/ Msimamo wa Iran wa Kuunga Mkono Palestina Ni Miongoni mwa Nguzo Kuu za Umoja

    Sheikh Naeem Qassem:

    Uvamizi wa Wazayuni Dhidi ya Qatar Ni Sehemu ya Mradi wa "Israeli Kubwa"/ Msimamo wa Iran wa Kuunga Mkono Palestina Ni Miongoni mwa Nguzo Kuu za Umoja

    Akiwahutubia viongozi wa nchi za Kiarabu, Sheikh Qassem alisema: "Pendekezo langu la pili ni hili: Msisimame pamoja na Israel, msiisaliti Harakati ya Mapambano kwa kujaribu kuipokonya silaha au kukubali masharti ya utawala wa Kizayuni."