Nuru
-
Kumbukumbu ya Shahidi Sayyid Ali Khamenei | Ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu Ndiyo Siri ya Athari ya Kudumu
Ujumbe huu unaotolewa katika mnasaba wa kumbukumbu ya Shahidi Ali Khamenei unasema hivi kuwa "Ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu ndiyo msingi wa kudumu kwa matendo mema", huku ukisisitiza kwamba athari ya kweli huzaliwa na nia safi ya kumtumikia Allah (swt).
-
Kituo cha Imam Sajjad (as) Kigoma kinaendelea kuelimisha vijana na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (as)
Chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mkuu, Sheikh Hussein Moshi Abdallah, Kituo cha Imam Sajjad (as) kilichopo Kasuko, mkoani Kigoma, kinaendelea kutoa elimu ya dini kwa vijana na kuinua bendera ya Ahlul-Bayt (as) nchini Tanzania.
-
Andiko Kamili la Khutba ya Fadak ya Bibi Fātima Zahra (a.s) pamoja na tarjama yake
1. Mwanzo wa Khutba – Malalamiko kuhusu dhulma na msimamo wa watu Kisha hamkungoja hata kidogo ili moyo uliokuwa umejeruhiwa utulie, na hali ile ngumu iwe nyepesi. Bali mliongeza kuni kwenye moto, mkaufukuzia upepo ili uongezeke kuwaka. Mlikuwa tayari kuitikia mwito wa Shetani, mkijiandaa kuzima nuru angavu ya dini ya Mwenyezi Mungu, na kuondoa Sunna za Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliyechaguliwa. Kwa kisingizio cha maslahi, mlikuwa mkila kijuujuu na kuficha nia zenu. Mlikuwa mkifanya njama nyuma ya vilima na miti dhidi ya familia yake na watoto wake. Na sisi tulipaswa kustahimili mambo haya yenye uchungu kama kisu chenye makali makali, au mkuki unaopenya tumboni.