Naibu wa Kitengo cha Utamaduni, Jamii na Hija wa Mkoa wa Khorasan Razavi, Hojjatoleslam Ali Asgari, amesema kuwa idadi ya mazuwwari katika siku za mwisho za mwezi Safar imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka uliopita. Kwa kuzingatia likizo zinazokaribia, inatarajiwa kuwa idadi ya mazuwwari itafikia takriban milioni 8.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s), akiwa katika makao makuu ya Jumuiya ya Maulamaa wa Senegal, amesisitiza juu ya umuhimu wa umoja wa Kiislamu na kuimarisha uwezo wa kielimu na kidini katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesema: “Umoja wa Kiislamu Ni Njia ya Kufikia Mamlaka ya Kiulimwengu”