Ikumbukwe kuwa, baada ya kurejea madarakani, Taliban ilifuta rasmi Sheria ya Hali ya Kiraia ya Waislamu wa Kishia, na kuondoa vitabu vyote vya Fiqh ya Ja’fari kutoka vyuo vikuu, shule na maktaba za serikali. Kundi hilo limekuwa likisisitiza kwamba sheria za Afghanistan lazima zitekelezwe kwa mujibu wa Fiqh ya Kihanifi pekee.
Vyombo vya Habari vya Pakistan vimeripoti kuwa mchakato wa kuwatimua wahamiaji wa Afghanistan bila hati za ukazi wa kisheria kutoka nchi hii umepangwa kuanza leo Jumanne (Aprili 1).
Human Rights Watch, katika ripoti yake ya hivi punde kuhusu wahamiaji wa Afghanistan nchini Pakistan, ilionyesha wasiwasi wake kuhusu kufukuzwa kwa lazima kwa wahamiaji hao.