Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S.) - ABNA -; Human Rights Watch,katika ripoti yake ya leo (Jumatano, Machi 19) kuhusu wahamiaji wa Afghanistan nchini Pakistan, ilionyesha wasiwasi wake kuhusu kufukuzwa kwa lazima kwa wahamiaji hao.
Mwanzoni mwa ripoti hii, inasemekana: Mamlaka za Pakistan zimezidisha shinikizo kwa wakimbizi wa Afghanistan kurejea Afghanistan, ambapo wanakabiliwa na mateso na Taliban na wanakabiliwa na hali mbaya sana ya kiuchumi.
Ikirejelea hali mbaya ya Haki za Binadamu nchini Afghanistan baada ya Taliban kuchukua hatamu, ripoti hii iliendelea: Wale wanaorejea nchini wanakabiliwa na ukosefu wa ajira, mfumo wa afya ulioharibika, na ukosefu wa misaada ya kigeni.
Bi. Elaine Pearson, Mkurugenzi wa Asia wa Human Rights Watch alisema katika ripoti hii: Mamlaka za Pakistan zinapaswa kuacha mara moja kuwashinikiza Waafghanistan kurejea nchini mwao. Na kwa wale ambao wanakabiliwa na kufukuzwa, wapewe nafasi ya kutafuta hifadhi.
Aliendelea: Kundi la Taliban nchini Afghanistan lazima lizuie hatua zozote za kulipiza kisasi dhidi ya waliorejea na kufuta vitendo vinavyokiuka Haki za Binadamu dhidi ya Wanawake na Wasichana (Mabinti).
Katika ripoti hii, limetajwa wimbi la hapo awali la kufukuzwa kwa wahamiaji wa Afghanistan kutoka Pakistan, ambalo lilitokea Septemba 2023 hadi Januari 2024, na akasema kwamba katika tarehe hii, zaidi ya Waafghani 800,000 walirudishwa Afghanistan. Ingawa idadi kubwa yao walizaliwa Pakistan au walikuwa wameishi katika nchi hiyo kwa miongo kadhaa.
Imeelezwa zaidi: Tangu Novemba 2024, mamlaka ya Pakistan imezidisha shinikizo la kuwafukuza Waafghanistan. Zaidi ya 70% ya wanaorejea ni Wanawake na Watoto, ikiwa ni pamoja na wasichana ambao wana umri wa kwenda shule lakini hawangeweza kupata elimu nchini Afghanistan.
Kisha, katika ripoti hii, imejadiliwa mifano ya mapungufu na matatizo ya wahamiaji wa Afghanistan nchini Pakistan.
Your Comment