gesi
-
Kwa maelekezo ya Rais, miradi 5 ya maendeleo ya Wizara ya Mafuta ya Iran yazinduliwa
Iran yazindua miradi mitano ya kimkakati ya sekta ya mafuta na gesi yenye thamani ya dola milioni 350, inayolenga kuongeza uzalishaji wa gesi asilia hadi mita za ujazo milioni 32 kwa siku, kuimarisha miundombinu ya nishati na kupunguza gesi zinazopotea kutokana na uchomaji.
-
Pezeshkian: Mashambulizi ya Kijeshi ya Marekani na Utawala wa Kizayuni Dhidi ya Iran Yamehatarisha Usalama wa Nishati na Uchumi wa Dunia
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, akihutubia Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Jukwaa la Nchi Zinazouza Gesi Asilia, uliofanyika jijini Moscow, alitoa heshima kwa kumbukumbu ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Ali Khamenei (Marehemu), akisisitiza kuwa mipango na uungwaji mkono wake vilikuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha jukwaa hilo. Aidha, akizungumzia matokeo ya mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, Pezeshkian alisema kuwa vikwazo vya upande mmoja pamoja na kuzingirwa kwa njia za baharini na angani kwa nchi hiyo ni tishio kwa uthabiti wa masoko ya nishati. Alitoa wito wa kulaani hatua hizo na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana nazo.
-
CNBC: Thamani ya Uwekezaji wa Trump katika Sekta ya Mafuta Yaongezeka Wakati wa Vita vya Iran
Uchambuzi wa CNBC umebaini kuwa thamani ya hisa na uwekezaji wa Rais wa Marekani, Donald Trump, katika kampuni za mafuta na gesi iliongezeka katika miezi sita ya mwanzo ya vita vya Iran.
-
Bei ya gesi Ulaya yavuka dola 800 kwa kila mita za ujazo 1,000
Bei ya gesi katika masoko ya Ulaya imepanda na kuvuka kiwango cha dola 800 kwa kila mita za ujazo 1,000, huku viwango vya gesi vilivyohifadhiwa katika vituo vya Ulaya vikipungua kwa kasi.
-
Kiongozi wa Iran Afichua Malengo ya Marekani Juu ya Utajiri wa Taifa la Iran
Imam Khamenei amesema Iran inalengwa na Marekani kutokana na utajiri wake wa asili na nafasi yake ya kijiografia, akibainisha kuwa mafuta, gesi na madini ya thamani ni miongoni mwa vivutio vinavyoifanya Iran kuwa shabaha ya tamaa ya kibeberu. Kauli hiyo aliitoa wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.