kisasa
-
Ustadh Sayyid Mojtaba Nurmufidi amesisitiza:Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani;
Alijitolea maisha yake yote katika utafiti,kuimarisha na kukuza elimu ya Fiqhi, pamoja na kulinda na kutetea mafundisho ya Madhehebu ya AhlulBayt(as)
Mwalimu wa masomo ya juu ya Fiqhi (Dars-e Kharij) katika Chuo Kikuu cha Kidini cha Qum, ambaye pia ni mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Masomo ya Fiqhi ya Kisasa, ametoa salamu za rambirambi kufuatia kufariki dunia kwa Ayatullah Al-Udhma Hussein Wahid Khorasani. Ameeleza kuwa msiba huo ni pigo kubwa katika misingi ya elimu ya Fiqhi na ulimwengu wa Kishia.
-
Mufti wa Misri Atoa Onyo Kuhusu Mkanganyiko wa Taarifa: Ni Muhimu Kuzitafsiri Upya Thamani za Kiislamu kwa Lugha ya Kisasa
Nazir Muhammad Ayyad, Mufti wa Jamhuri ya Misri, akisisitiza umuhimu wa kuzitafsiri na kuziwasilisha upya misingi na thamani za Kiislamu kwa lugha ya zama hizi, pamoja na kuziunganisha na masuala ya vyombo vya habari vya kidijitali, mitandao ya kijamii na akili mnemba (AI), amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha uelewa wa kijamii na kukabiliana na mkanganyiko wa taarifa unaoikabili dunia ya leo.
-
Ayatullah Haidari katika mahojiano na ABNA:
Shahidi Nasrallah Alitaka Fiqhi ya Kisiasa ya Shia Ifafanuliwe kwa Lugha ya Kisasa kwa Vijana; Simulizi ya Sayyid wa Muqawama kuhusu “Wimbi la Ushia”
Ayatullah Mohsen Haidari, akieleza kuhusu msisitizo wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah juu ya umuhimu wa kuandaa na kuendeleza fasihi na istilahi za kisasa katika uwanja wa Fiqhi ya Kisiasa ya Shia, amesema: “Vyanzo muhimu vya Fiqhi ya Kisiasa ya Shia vimeandikwa kwa lugha na mtindo wa zamani. Jambo hili limechangia kujitokeza kwa baadhi ya mashaka na maswali kuhusu Wilayat al-Faqih, Serikali ya Kiislamu na ushiriki wa kisiasa miongoni mwa vijana. Kwa sababu hiyo, Shahidi Nasrallah alisisitiza umuhimu wa kufafanua dhana hizi kwa lugha ya kisasa na inayoeleweka kwa kizazi kipya.”
-
Walinzi wa Mapinduzi: Tumeiangamiza ndege isiyo na rubani ya MQ-1 juu ya Mlango Bahari wa Hormuz
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran limesema mfumo wake wa ulinzi wa anga umefanikiwa kuikamata na kuiangamiza ndege ya kisasa isiyo na rubani aina ya MQ-1 iliyokuwa ikiruka juu ya Mlango Bahari wa Hormuz.
-
“Bao la kujifunga” la dola milioni 4: Vikosi vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia vyaangusha drone yao kwa bahati mbaya
Vikosi vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia vimeripotiwa kuangusha kwa bahati mbaya ndege yao ya kisasa isiyo na rubani aina ya CH-4, yenye thamani ya takriban dola milioni 4, wakidhani kuwa ilikuwa ya Ansarullah.
-
Noor Centre Dar es Salaam Yaandaa Kikao Maalum cha Kujadili Utume wa Mtume (saw) Katika Dunia ya Kisasa
Sheikh Ali Asad Esmail aongoza kikao maalum cha “Utume wa Mtume (saww) Katika Dunia ya Kisasa” kilichoandaliwa na Noor Centre Dar es Salaam, Tanzania.
-
Mafanikio 5 ya Iran katika Sekta ya Anga na Usafiri wa Anga kwa Kutumia Akili Bandia
Wataalamu na mafundi wa Iran wamefanikiwa kutumia akili bandia katika sekta ya anga na usafiri wa anga, hatua inayolenga kuipeleka nchi hiyo kutoka katika hatua ya uhandisi wa kubuni upya teknolojia hadi katika ubunifu wa kisasa unaotegemea akili bandia.
-
Msemaji wa IRGC: Akili bandia ilishindwa katika vita vya adui dhidi ya Iran
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Hossein Mohebi, amesema adui alitumia teknolojia za kisasa za kijeshi, akili bandia, mifumo ya uongozi na data za satelaiti na ndege zisizo na rubani katika kujaribu kuchambua uwezo wa Iran na kubaini malengo yake, lakini hatimaye ilishindwa na nguvu ya taasisi, imani, umoja, mshikamano na utashi wa wananchi wa Iran.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Ubunifu wa Iran umebadilisha mizani ya uwanja wa vita
Waziri wa Ulinzi na Msaada kwa Jeshi la Iran amesema kuwa katika vita vya hivi karibuni, adui alitumia teknolojia za hali ya juu zaidi duniani, lakini ubunifu na uwezo wa ndani wa Iran uliweza kubadilisha mizani ya uwanja wa vita.
-
Brigedia Jenerali Ibn al-Ridha: Vikwazo na Vita Vimekuwa Chachu ya Maendeleo ya Kiteknolojia ya Ulinzi Nchini Iran
Naibu Waziri wa Ulinzi na Msaada wa Majeshi ya Iran, Brigedia Jenerali Sayyid Majid Ibn al-Ridha, amesema vikwazo na vita vimekuwa miongoni mwa sababu zilizochochea maendeleo makubwa ya kiteknolojia katika sekta ya ulinzi ya Iran.
-
Marekani yaiondoa ndege yake ya upelelezi MQ-4C Triton kutoka Jordan kuelekea Italia baada ya mashambulizi ya Iran
Ripoti zinaeleza kuwa Marekani imeiondoa ndege yake ya kisasa ya upelelezi aina ya MQ-4C Triton kutoka Jordan na kuihamishia Italia, hatua inayokuja baada ya mashambulizi ya Iran dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Rubani wa Marekani Adai Kuona “Ndege zisizo na Rubani za Umbo la Jellyfish” Katika Anga ya Iran
Rubani wa ndege ya kivita aina ya F-15 ya Marekani amedai kuwa aliona kundi la ndege zisizo na rubani za Iran zikisafiri kwa mpangilio maalumu unaofanana na umbo la “jellyfish”, madai ambayo yamezua mjadala katika duru za kiintelijensia za Marekani kuhusu uwezo wa teknolojia ya droni za Iran.
-
Admirali Sayyari: Vikosi vya Iran Vinatumia Vifaa vya Kisasa Vinavyoendana na Teknolojia za Hali ya Juu
Msaidizi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, Admirali Habibollah Sayyari, amesema kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vina vifaa vya kisasa na vipo tayari kukabiliana na tishio lolote, huku akisisitiza kwamba adui yeyote atakayeshambulia Iran atakabiliwa na jibu kali zaidi kuliko hapo awali.
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s): Imam Khomeini (r.a) Aliirejesha Dini Kutoka Pembezoni Hadi Kiini cha Jamii na Utawala
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), Ayatullah Reza Ramadhani, amesema kuwa Imam Khomeini (r.a) aliirejesha dini kutoka pembezoni hadi kuwa kiini cha maisha ya kijamii na mfumo wa utawala, akithibitisha kuwa dini inaweza kuwa msingi wa uongozi, haki ya kijamii na ujenzi wa ustaarabu wa kisasa.