Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuharibu mifumo ya kurushia makombora ya HIMARS nchini Kuwait na kushambulia maeneo ya vikosi vya Marekani pamoja na malengo iliyoyataja kuwa yanahusishwa na wapinzani wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Tarehe 11 Februari 2026, maelfu ya Wairani walikusanyika kuonyesha mshikamano wao na taifa na kuthibitisha kwamba Marekani ni adui wa Umma wa Kiislamu.
Tukio hili linaonyesha wazi kwamba mbinu za adui hazina nafasi mbele ya mshikamano wa wananchi wa Iran na jitihada za kuharibu taifa hilo hazina mafanikio.
Hashd Al-Shaabi ya Iraq imefanikiwa kugundua na kuharibu handaki na maficho ya ISIS Mashariki mwa Salahuddin kwa kushirikiana na jeshi la Iraq, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuzuia kurejea kwa makundi ya kigaidi katika eneo hilo.