Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Vikosi vya Hashd Shaabi vya Iraq vimetangaza kugundua na kuharibu handaki na maficho kadhaa ya wanachama wa kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) mashariki mwa mkoa wa Salahuddin.
Operesheni hiyo imefanyika katika mfumo wa oparesheni ya pamoja ya kiusalama kwa ushirikiano na vikosi vya jeshi la Iraq, kwa lengo la kusafisha maeneo yaliyochafuliwa na kuzuia kurejea kwa harakati za seli za kigaidi.
Your Comment