kujibu
-
IRGC yadai kulenga Kambi ya Anga ya Amir Hassan nchini Jordan kwa makombora na ndege zisizo na rubani
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), vikosi vyake vimedai kulenga majukwaa ya makombora, maghala ya mafuta na maeneo ya kuhifadhia silaha katika Kambi ya Anga ya Amir Hassan nchini Jordan, katika kile ilichokieleza kuwa ni hatua ya kujibu ukiukaji uliofanywa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran: Ukiukaji wa Ahadi za Marekani Utakabiliwa na Hatua za Kujibu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema Iran haijaomba mazungumzo na Marekani, akisisitiza kuwa sera ya Jamhuri ya Kiislamu inategemea kanuni ya "ahadi kwa ahadi" na kwamba ukiukaji wowote wa ahadi za Washington utakabiliwa na jibu la Iran.
-
Jenerali Ismail Qa'ani: Gaza pia ina “Tufani” yake; msidharau uwezo wa Muqawama
Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Jenerali Ismail Qa'ani, ameonya kuwa Gaza pia ina uwezo mkubwa wa kujibu mashambulizi, akisema kuwa kupuuza maonyo ya Muqawama kunaweza kusababisha hasara kubwa zaidi.
-
Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa Yatangaza Kushambulia Kambi za Marekani Kufuatia Uchokozi Dhidi ya Iran
Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (s) yamesema vikosi vya Jeshi la Iran na Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu vimeshambulia baadhi ya kambi za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, vikieleza kuwa hatua hiyo ni jibu kwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya kusini mwa Iran.