kukabidhi
-
Mwakilishi wa Nujaba Iran: Hatutaacha uwanja wa mapambano wala kukabidhi silaha zetu
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Harakat al-Nujaba nchini Iran, Hujjatul-Islam Sayyid Abbas Mousavi, amesema kuwa kwa misingi ya wajibu wa kidini, uwajibikaji na uaminifu kwa kiongozi wao aliyefariki shahidi, hawataondoka katika uwanja wa mapambano wala kukabidhi silaha zao, akisisitiza kuwa wataendelea na njia yake.
-
Kwa nini Hizbullah ya Lebanon ilikataa kukabidhi maeneo ya miinuko ya Ali al-Taher?
Pendekezo ambalo kwa msingi wake Hizbullah ingeyaondoa majeshi yake katika maeneo ya miinuko ya Ali al-Taher na Jeshi la Lebanon kuchukua nafasi yake, kwa mtazamo wa Hizbullah si mpangilio wa kijeshi wa uwanjani tu, bali linaweza kuunda mfano wa kulazimisha madai zaidi ya utawala wa Kizayuni katika maeneo mengine ya Lebanon.
-
Osama Hamdan: Kuzungumzia kukabidhi silaha za Muqawama ni jambo lisilo na maana
Katika mwendelezo wa matamko yanayofichua malengo ya kweli ya utawala wa Kizayuni wa Israel, mwanachama mwandamizi wa Harakati ya Hamas, Osama Hamdan, amesisitiza kuwa mazungumzo kuhusu kukabidhi silaha za Muqawama hayana msingi wowote. Ameeleza kuwa wakati Israel inakiuka ahadi zake zote, lengo lake kuu linaendelea kuwa ni kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.
-
Sheikh wa Kisunni Lebanon: Tukisikia Hizbullah inataka kuweka silaha chini, sisi Wasunni tutapinga vikali
Sheikh Maher: Kuwasilisha (kukabidhi) silaha ni usaliti; usaliti kwa Mungu na Mtume (s.a.w) na sisi tunaelewa kabisa hilo.