Alielekeza maneno yake kwa Rais Joseph Aoun, akisema:
"Uliwaambia watu wa Muqawama kuwa waitegemee Serikali – lakini haukusema ni Serikali ipi hiyo? Watu wetu hawako tayari kuwa wahanga wa wauaji ambao watawatendea kama walivyowatendea Wapalestina."
Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahrain amesema: A'"shura inatolewa kila mwaka katika vyombo vya habari vya Bahrain kama ishara ya uhuru na uvumilivu wa kidini, lakini kivitendo wafuasi wa Kishia wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na vikwazo vikali, kuanzia kukamatwa na kuandikiwa wito hadi kuharibiwa maeneo ya kidini na mashinikizo ya kubadili mavazi ya kidini.