Sudan kwa mwaka wa tatu mfululizo imeorodheshwa juu kabisa katika orodha ya migogoro ya kibinadamu duniani.Nchi nyingine zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo ni pamoja na: Myanmar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mali, Burkina Faso, Lebanon, Afghanistan, Cameroon, Chad, Colombia, Niger, Nigeria, Somalia, Syria, Ukraine na Yemen.
Mamlaka za nchi mbili, Somalia na Sudan, zimekataa katakata pendekezo na mpango wowote kuhusu uhamisho wa Wapalestina wanaoishi Gaza hadi katika eneo la nchi hizi za Kiafrika.