ukraine
-
Urusi, mataifa ya Ulaya zakubaliana kuhusu mpango wa amani wa Ukraine
Viongozi wa Urusi, Ujerumani na Ufaransa wamekubaliana katika mazungumzo yao mjini Moscow kupanga mpango wa kumaliza mapigano nchini Ukraine wakati waasi wakifanya mashambulizi makubwa upande wa mashariki mwa nchi hiyo.
-
Jeshi la Ukraine laondoka katika uwanja Donetsk
Jeshi la Ukraine limeondoka katika uwanja mkuu wa ndege katika mji wa Donetsk unaodhibitiwa na waasi, baada ya mapigano makali yaliyouwa wanajeshi wa serikali wasiopungua 10 na kuwajeruhi wengine 16.
-
Mzozo wa Ukraine wapamba moto
Wanajeshi wa Ukraine wamefyetuliana mizinga na waasi mashariki ya Ukraine.Serikali ya mjini Kiev inadai wanajeshi wa Urusi walishiriki katika mapigano hayo na kwa namna hiyo kuzidisha makali ya mzozo huo.
-
Mogherini asema: Ulaya itaendeleza vikwazo kwa Urusi
Mogherini amesema wataendelea na msimamo wao hadi Urusi itekeleze makubaliano ya amani yaliofikiwa mwezi Septemba.
-
Majeshi ya Urusi yaingia Ukraine
Jeshi la Ukraine limedai kiasi ya wanajeshi 700 kutoka Urusi wamevuka mpaka hii leo na kuingia mashariki mwa Ukraine ambako kunaendelea mapigano makali kati ya wanajeshi na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
-
Mawaziri wa Ulaya wakutana kujadili ugaidi na amani ya Ukraine
Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels, wakati mashambulizi mjini Paris na kugunduliwa kwa wapiganaji wa Jihadi nchini Ubeligiji, vikigonga vichwa vya habari.
-
Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu amani ya Ukraine
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameelezea wasiwasi wake kuhusu mapigano makali yanayoripotiwa mashariki mwa Ukraine katika uwanja wa ndege wa Donetsk na kutaka ghasia hizo kukomeshwa mara moja
-
Urusi yaomba mapigano yasitishwe kabla ya mkutano kuhusu amani ya Ukraine
Urusi imetoa wito wa usitishaji mara moja wa uhasama mashariki mwa Ukraine leo na kuonya kwamba serikali ya Ukrane, mjini Kiev inatafuta suluhisho la kijeshi katika mzozo huo.
-
Ukraine yajiandaa kukabiliana na waasi kwa vita
Imejiandaa kukabiliana na waasi wa nchi hiyo kwa vita, licha ya kuendelea kwa mpango mazungumzo ya amani ya Berlin na mkutano kuhusu mzozo huo ukitarajiwa kufanyika wiki ijayo Kazakhstan.
-
Hollande: vikwazo dhidi ya Urusi vinaweza kuondolewa
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema leo kuwa vikwazo vya nchi za Magharibi vinavyoendelea kuiathiri Urusi vinapaswa kuondolewa kama hatua zitapigwa katika ufumbuzi wa mgogoro wa Ukraine.