vurugu
-
Janga la Kibinadamu Gaza; Watoto Yatima Katika Hali ya Ndoto Mbaya
Janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza limeharibu maisha ya maelfu ya watoto. Watoto hawa wamekuwa wakikabiliana na hali ya kukimbia, njaa, kifo cha wapendwa, na vurugu za kutisha kwa takriban miaka miwili. Ripoti zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 65,000 wamefariki Gaza, huku maelfu ya watoto wakipoteza wazazi wao. Hali hii ya ukosefu wa usalama na mahitaji ya msingi inatengeneza athari kubwa za kimahusiano na kisaikolojia kwa vizazi vijavyo, na kufanya msaada wa haraka wa kimataifa kuwa jambo la dharura. Watoto hawa yatima sasa wanahitaji hifadhi, chakula, huduma za afya na msaada wa kisaikolojia ili kuweza kuendelea na maisha yao.
-
Mwenyekiti wa Chama cha Majlis Ittehad-ul-Muslimeen nchini India;
Ameonesha msimamo wake kufuatia mjadala uliyoibuka dhidi ya bango lenye maandishi “Nampenda Muhammad”.
Kiongozi wa chama cha Majlis Ittehad-ul-Muslimeen nchini India, akijibu mzozo ulioibuka kutokana na mabango yenye maandishi “Nampenda Muhammad” katika jimbo la Uttar Pradesh, ameishutumu serikali ya India na viongozi wa eneo hilo kwa kuweka vizuizi vya kibaguzi na vya upendeleo.
-
Juhudi zinaendelea kuiadhibu Israel katika michezo kutokana na vita yake dhidi sya Gaza
Wakati mbio kubwa za baiskeli nchini Hispania zilikumbwa na vurugu za waandamanaji waliopinga ushiriki wa timu ya Israel, mataifa kadhaa ya Ulaya yametishia kususia tukio maarufu la burudani endapo Israel itaruhusiwa kushiriki.