20 Februari 2025 - 19:57
Ziyad al-Nakhala: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni egemeo la makundi ya muqawama

Ziyad Al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni egemeo na muungaji mkono wa makundi ya muqawama.

Ziyyad al-Nakhala amesema hayo hapa mjini Tehhran katika mazunguumzo yake na Ali Akbar Ahmadiyyan, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran na kubainisha kwamba, 'makundi yote amilifu yamo katika ushindi katika kuendeleza muqawama na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina pia amesema kuwa, ushindi mkubwa wa muqawama wa Gaza ni mdaiwa wa muqawama wa Mujahidina wa Palestina, Lebanon, Yemen na Iraq na uungaji mkono wa daima wa Jamhuri ya Kiislamu.

Ziyad al-Nakhala ameashiria "umoja na mshikamano" wa kisiasa wa makundi ya muqawama ya Palestina na Lebanon na kusema: "Makundi yote amilifu yamepata ushindi pamoja na muqawama na Jamhuri ya Kiislamu."

Kadhalika kiongozi huyo wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina amesema bayana kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ni mlima ambao makundi yote ya upinzani yanautegemea na kuuegemea.

Kwa upande wake Ali Akbar Ahmadiyan, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema, mapambano ya wapiganaji wa Jihad na Hamas na subira ya watu wa Gaza yalifanyika kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa amesema kuwa, muqawama na subira ya wananchi wa Gaza dhidi ya adui Mzayuni na Marekani imeweza kuwa na taathira katika fikra za watu wa dunia, Waislamu na wasio Waislamu.

342/