Tukio hilo, lililotangazwa siku ya Jumanne, limekuwa mara ya kumi na tano ambapo ndege za aina hiyo zimeangushwa na vikosi vya ulinzi wa anga vya Yemen tangu kuanza kwa mapambano ya "Ushindi Ulioahidiwa" na "Jihad Tukufu."
Droni moja ya MQ-9 Reaper inagharimu takribani dola milioni 33.
Jeshi la Yemen lilianzisha mapambano hayo mnamo Oktoba 2023 baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza na Lebanon kwa himya ya Marekani.
Jeshi la Yemen pia linatekeleza operesheni hizo kukabiliana na mahsmabulizi ya utawala wa Israel, Marekani, na Uingereza dhidi ya miundombinu ya ulinzi na raia wa taifa hilo.
Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya vikosi vya Yemen inaendelea kufanya kazi kikamilifu na iko tayari kukabiliana na uvamizi wowote wa kigeni.
Jeshi la Yemen limesisitiza kuhusu azma yake ya kusimama na watu wa Palestina na Lebanon, kama sehemu ya mstari wa mbele wa pamoja dhidi ya uchokozi wa Israel na Marekani.
Mbali na kukabiliana na vitisho vya anga, vikosi vya Yemen viliangazia pia utayari wao wa kufuatilia harakati za maadui katika Bahari Nyekundu na Bahari ya Kiarabu.
Hivi karibuni, ama vikosi hivyo au maafisa waandamizi wa Yemen wameonya Israeli na Marekani kuhusu kuendelea na uchokozi dhidi ya ardhi za Palestina, Lebanon na Yemen.
Zaidi ya hayo, serikali ya Sana’a imeitaka jumuiya ya kimataifa kuziwajibisha Tel Aviv na Washington kwa vitendo vyao vya uchokozi, huku ikionya kuwa mashambulizi yanayoendelea yanaweza kuwa na athari mbaya kwa pande zote zinazohusika.
342/
Your Comment