5 Machi 2025 - 22:42
Source: Parstoday
Hamas: Kufunga vivuko vya Ukanda wa Gaza ni jinai ya kivita

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesina HAMAS imelaani kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kufunga kwa siku tatu mfululizo vivuko vya Ukanda wa Gaza na kuitaja hatua hiyo kuwa inashadidisha kukiukwa makubaliano ya kusitisha mapigano na ni jinai ya kivita.

Hamas imetoa taarifa na kutangaza kuwa kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kuendelea kufunga vivuko vya Ukanda wa Gaza na kuzuia kuingia misaada ya kibinadamu na bidhaa mbalimbali katika eneo hilo ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano na jinai mkabala wa haki ya raia wa Kipalestina. 

Hamas imesisitiza kuwa hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni ni njama iliyoratibiwa ili kuwasababishia njaa raia wa Kipalestina na kuzidisha maafa ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza ili kufikia malengo yake ya kisiasa. 

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imezitaka Umoja wa Mataifa, taasisi za haki za binadamu na jamii ya kimataifa zichukue hatua haraka iwezekanavyo ili kusitisha vitendo hivyo vilivyo kinyume cha sheria na ziwaadhibu viongozi wa utawala wa Kizayuni kama watenda jinai za kivita. 

Hamas pia imesisitiza juu ya ulazima wa kutolewa mashinikizo ya kimataifa kwa Israel ili misaada ya kibinadamu, suhula za kitiba na vifaa vingime muhimu vifikishwe haraka Ukanda wa Gaza.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha