Viongozi wa nchi za Kiarabu walioshiriki katika mkutano wa dharura wa viongozi wa Kiarabu uliofanyika jana usiku huko Cairo, Misri katika taarifa yao ya mwisho wamepasisha mpango wa Misri wa kuijenga upya Gaza na kusisitiza kuhusu umuhimu wa kuilinda Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa umoja.
Mkutano wa Cairo pia umesisitiza kuhusu kipaumbele cha kukamilishwa makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza ambacho kinakabiliwa na changamoto kubwa.
Taraifa ya mwisho ya mkutano wa viongozi wa Arab League pia imeashiria namna mpango wa Misri unavyolinda mfungamano uliopo kati ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, amani ni chaguo la kistratejia la Waarabu.
Taarifa hiyo vile vile imetilia mkazo msimamo wa Waarabu kwamba wanapinga jitihada zozote za kuwafukuza kwa nguvu Wapalestina kwa anwani yoyote ile.
Viongozi wa nchi za Kiarabu wamesisitiza mwishoni mwa mkutano wao wa dharura huko Cairo kuhusu dira ya ufumbuzi wa serikali mbili.
342/
Your Comment