7 Machi 2025 - 22:30
Source: Parstoday
Yemen: US kuiweka Ansarullah katika orodha ya ugaidi haina uhalali wowote

Afisa mmoja mwandamizi wa Yemen amepuuzilia mbali hatua ya Marekani ya kuitambua Harakati ya Muqawama ya Ansarullah kama kundi la kigaidi, akisema uamuzi huo hauna uhalali wowote.

Mohammed Ali al-Houthi, Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen alisema hayo jana Alhamisi na kuongeza kuwa, "Kufikishwa misaada ya kibinadamu Gaza ni muhimu zaidi kwetu kuliko uamuzi huo wa Marekani, ambao hauna uhalali."

Mtandao wa habari wa Al-Mayadeen umemnukuu Al-Houthi akishutumu kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, na kutaja kitendo cha kupindisha makubaliano ya kusitisha mapigano kama "ugaidi wa Kimarekani."

Siku ya Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio alitangaza kwamba Washington kwa mara nyingine tena imeiorodhesha Harakati ya Ansarullah kama "shirika la kigeni la kigaidi."

Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesisitiza kuwa, kuingizwa Harakati ya Ansarullah katika orodha ya ugaidi ni kitendo kilichopitwa na wakati na hakina uhalali wowote isipokuwa kuutumikia Uzayuni. Ameeleza bayana kuwa: Lengo la Marekani ni kuzidisha mateso kwa taifa la Yemen na kulizuia taifa na majeshi ya nchi hiyo kuendelea kuliunga mkono taifa na kadhia ya Palestina.

Kabla ya hapo, Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ilitangaza katika taarifa yake kwamba, Marekani ambayo mikono yake imetapakaa damu za watu wasio na hatia, haina sifa wala ustahiki wa kuzihukumu nchi na mataifa mengine na kuziweka katika orodha ya ugaidi.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha