Likinukuu vyanzo vya usalama vya Palestina na wakazi wa Nablus, shirika rasmi la habari la Palestina la WAFA limesema Wapalestina watatu wamekamatwa na kuzuiliwa wakati wa uvamizi huo.
Magari ya kijeshi ya Israel yamevamia vitongoji vingi vya Wapalestina katika jiji hilo na kufyatua risasi za moto, maguruneti ya kupoozesha mwili na mabomu ya kutoa machozi.
Video zilizosambaa mitandaoni zinaonesha Wazayuni hao maghasibu mapema leo Ijumaa wakiuchoma moto msikiti mmoja katika mji wa Nablus.
Hii si mara ya kwanza kwa Wazayuni kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu katika mji huo mkongwe wa kihistoria wa Wapalestina.
Hivi karibuni pia, Walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali ya kufurutu ada walivamia msikiti mmoja na kuvunjia heshima Qurani Tukufu katika mji huo wa Nablus.
Makundi ya Muqawama wa Kiislamu yametoa mwito kwa Wapalestina wote kuihami misikiti na tasisi za kidini, huku yakitoa mwito kwa mashirika ya kimataifa kutekeleza wajibu wao wa kuwawabebesha dhima Wazayuni kwa jinai zao hizo.
342/
Your Comment