7 Machi 2025 - 22:34
Source: Parstoday
70 wauawa katika mapigano baina ya pande kinzani Syria

Zaidi ya watu 70 wameripotiwa kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa nchini Syria kutokana na mapigano makali kati ya wanamgambo wa kundi la kigaidi linalotawala la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) na makundi ya Muqawama ya wananchi huko magharibi mwa nchi hiyo.

Mehr News imeripoti habari hiyo na kueleza kuwa, asasi inayojiita 'Shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria' (SOHR) imesema katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X leo Ijumaa kwamba, waliopoteza maisha waliuawa kwenye pwani ya Syria baada ya wanamgambo wa Hay’at Tahrir al-Sham kuzingirwa na kuvamiwa.

Kundi hilo la kufuatilia vita lenye makao yake makuu Uingereza limesema: Katika mji wa pwani wa Jableh na vijiji vya karibu katika Mkoa wa Latakia, watu 48 waliuawa katika mapigano hayo.

Syrian Observatory for Human Rights (SOHR) imesema, mashambulizi hayo yaliyoratibiwa yalikuwa makubwa zaidi dhidi ya watawala wapya wa Syria tangu Rais Bashar al-Assad alipopinduliwa mapema Disemba mwaka jana.

70 wauawa katika mapigano baina ya pande kinzani Syria

Kadhalika wanamgambo 16 wa Tahrir al-Sham waliuawa wakati wa mapigano hayo jana Alkhamisi katika jimbo la Latakia, ambalo idadi kubwa ya wakazi wake ni Waislamu wa Alawi na Shia.

Mamlaka za ndani mkoani Latakia na Tartus zimetangaza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku, huku mapigano yakichachamaa.

Haya yanaripotiwa katika hali ambayo,  vikosi vya nchi kavu vya utawala haramu wa Israel vimeendelea kufanya uvamizi wa "kina kabisa" ndani ya ardhi ya Syria, vikilenga maeneo kadhaa katika mikoa ya kusini-magharibi ya Quneitra na Dara’a.

Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (GCC) limetoa mwito wa kuchukuliwa "hatua madhubuti" ili kukomesha mashambulizi ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Syria.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha