9 Machi 2025 - 22:07
Source: Parstoday
Kiongozi Muadhamu: Iran inakataa kabisa sisitizo la kufanya mazungumzo na madola ya kibabe

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyid Ali Khamenei, amesema kuwa sisitizo la baadhi ya madola ya kibabe juu ya kufanyika mazungumzo na Iran halilengi kutatua matatizo.

Ayatullah Khamenei aliyasema haya katika mkutano na wakuu wa mihimili mitatu ya dola na maafisa wa mfumo mzima wa Iran jijini Tehran siku ya Jumamosi.

Kiongozi Muadhamu ameendelea kusema kuwa: "Sisitizo la baadhi ya serikali za kibabe juu ya mazungumzo si kwa ajili ya kutatua matatizo, bali ni njia ya kulazimisha matarajio yao binafsi."

Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitatimiza matarajio yao.

Aidha amesisitiza kuwa madola haya ya kibabe hayalengi tu kujadili suala la nyuklia, bali yanatumia mazungumzo kama "njia ya kuibua matarajio mapya" katika nyanja kama vile uwezo wa ulinzi wa Iran na uwezo wake wa kimataifa, mambo ambayo Iran haitayakubali kamwe.

Kiongozi Muadhamu amebainisha kuwa madola hayo yanaibua suala la mazungumzo ili kushinikiza maoni ya umma, na ili yadai kuwa yako tayari kwa mazungumzo na kwamba eti  Iran ndiyo inayokataa.

Ayatullah Khamenei pia amezikosoa nchi za Ulaya kwa kutoa madai ya uongo dhidi ya Iran, akisema kwamba dai lao kuwa Iran haijatekeleza ahadi zake za nyuklia  "si la kimantiki."

Ayatullah Khamenei ameendelea kuzihutubu nchi za Ulaya hivi: "Mnasema Iran haijatekeleza ahadi zake za nyuklia. sawa, je, nyinyi mlitekeleza zenu? Hamkuzitimiza tangu mwanzo."

Kiongozi Muadhamu: Iran inakataa kabisa sisitizo la kufanya mazungumzo na madola ya kibabe

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Khamenei akiswalisha baada ya mkutano wake na maafisa wa mihimili mitatu ya dola

Kiongozi Muadhamu amebaini kuwa baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya 2015, nchi za Ulaya ziliahidi kufidia suala hilo, lakini zilishindwa kutimiza ahadi yao.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa misingi ya ustaarabu wa Magharibi inapingana na misingi ya Uislamu na "hatuwezi kuwafuata."

Ameendelea kusema kuwa: "Tunaweza na tunapaswa kunufaika na chochote chenye manufaa popote pale duniani, lakini hatuwezi kutegemea misingi ya ustaarabu wa Magharibi."

Kiongozi Muadhamu amebaini kuwa matendo ya mataifa ya Magharibi, ikiwa ni pamoja na ukoloni, uporaji wa rasilimali za mataifa mengine, mauaji ya halaiki, madai ya uongo kuhusu haki za binadamu na haki za wanawake, pamoja na viwango vyao vya undumakuwili katika masuala mbalimbali, vimeleta fedheha kwa ustaarabu wa Magharibi.

Ayatullah Khamenei amesema "[Dai la] uhuru wa maoni katika nchi za Magharibi si chochote zaidi ya uwongo."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha