1 Novemba 2024 - 06:42
Mazuwaru wanahuisha usiku wa Ijumaa ya mwisho katika mwezi wa Rabiul-Aakhar mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Kundi la waumini limekuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Rabiul-Aakhar mbele ya malalo yake takatifu mjini Karbala.

Mji mtukufu wa Karbala hupokea idadi kubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, na kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s). Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake hufanya kila iwezale katika kuhudumia mazuwaru.