Akizungumza kwa njia ya televisheni, Sayyid Abdul-Malik al-Houthi amesema: "Ikiwa Israel itafanikiwa kuangamiza juhudi za ukombozi wa Palestina, bila shaka itapanua uchokozi wake kwa nchi nyingine bila kizuizi."
Ameendelea kusema kuwa: "Wale wanaotegemea makubaliano na Israel wanapaswa kutambua kuwa Israel haizingatii ahadi, hata ikiwa zimehakikishwa na Marekani."
Kiongozi wa Ansarullah alikuwa akiashiria mataifa ya Kiarabu ya kanda ambayo yameingia katika makubaliano na utawala wa Israel chini ya upatanishi wa Marekani ambayo ni pamoja na Jordan, Misri Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Morroco na Sudan pamoja na Saudi Arabia ambayo iko chini ya mashinikizo ya kufikia mapatano kama hayo.
Matamshi hayo yamekuja baada ya utawala haramu wa Israel kuanzisha mashambulizi mkubwa ya mauaji ya halaiki dhidi ya Gaza mapema Jumanne, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa yameanza kutekelezwa Januari kwa lengo la kumaliza zaidi ya miezi 15 ya vita vya mauaji ya halaiki ambayo yamekuwa yakitekelezwa na Israel katika eneo hilo.
Kulingana na maafisa wa afya wa Palestina, watu 424 waliuawa katika mashambulizi ya Jumanne pekee, wakiwemo watoto 174 na wanawake 89. Zaidi ya watu 600 walijeruhiwa wakati vikosi vya Israeli viliposhambulia nyumba, misikiti na makazi ya waathirika.
Kiongozi wa Ansarullah wakati huo huo, amehoji hivi, "kwa nini nchi za Kiarabu na Kiislamu hazitoi msaada wa kijeshi kwa wapiganaji wa Palestina"?
Ameshauri nchi hizo kuwapatia silaha wapigania ukombozi wa Palestina kama njia ya kukabiliana na msaada mkubwa wa kijeshi kwa utawala huo kutoka Magharibi, hasa Marekani..
Amesema: "Muqawama wa Kipalestina unahitaji msaada wa kifedha na kijeshi; nchi za Kiarabu na Kiislamu zinapaswa kuwajibika kutoa msaada hu."
Al-Houthi pia amezitaka Uturuki, Misri, Jordan, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Tel Aviv ili kuudhoofisha kiuchumi.
Aidha amesema Yemen itaendeleza mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Israel kwa lengo la kuwatetea Wapalestina.
Amesema Jeshi la Yemen litakabiliana na hujuma yoyote ya Marekani dhidi ya nchi hiyo.
342/
Your Comment