19 Machi 2025 - 18:30
Source: Parstoday
'Waislamu wachukue msimamo wa maana dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni'

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq ya An-Nujabaa imelaani mashambulizi ya kinyama yaliyoanzishwa tena na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na kuwataka Waarabu na Waislamu duniani kote wachukue misimamo thabiti dhidi ya hujuma hizo.

An-Nujabaa imetoa taarifa na kueleza kwamba kuanzishwa tena kwa vita dhidi ya Ghaza na genge la wahalifu wa Kizayuni kwa uungaji mkono wa moja kwa moja wa Marekani kunatoa picha na taswira ya wazi kabisa ya uovu, udhalimu na ukatili, pamoja na ukiukaji wa maadili na akhlaqi za kiutu na mafundisho ya mbinguni, ambao watendaji wake mikono yao imetapakaa damu za raia na watoto wasio na hatia.

Harakati ya An-Nujabaa imeutahadharisha Umma wa Kiislamu na hasa mataifa ya Kiarabu kwamba, iwapo hayatachukua msimamo thabiti na unaostahiki, Ghaza itafutwa katika ramani na wahalifu wa kivita; na kubaki kuwa watazamaji tu wa taswira hiyo ovu ni aibu na fedheha kubwa kwa umma ambao heshima na utu wake unakanyagwa na kupondwa pondwa mbele ya macho yake katika ardhi ya Palestina.

Aidha, harakati  hiyo ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq mbali na kueleza kusikitishwa na ushirikiano wa siri na wa dhahiri wanaotoa baadhi ya Waarabu na Waislamu kwa utawala haramu wa Kizayuni, na huku ikisisitiza kwamba uthabiti na istiqama ya kupigiwa mfano ya Ghaza haitavunjwa, imewahutubu Wazayuni: "milango ya Jahannamu itafunguliwa kwenu nyinyi, waungaji mkono wenu na kila anayeridhishwa na matendo yenu".../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha