Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) -ABNA-; Yahya Saree, msemaji wa jeshi la Yemen, ametangaza kuwa Uwanja wa ndege wa Ben Gurion katika eneo la Palestina linalokaliwa la kwa mabavu la "Jaffa", umelengwa (umeshambuliwa) kwa Kombora la Balestiki la "Palestine 2" na kwamba (shabaha) lengo la operesheni hii lilifikiwa kwa mafanikio.
Msemaji wa jeshi la Yemen pia alitangaza utekelezwaji wa operesheni za makombora na ndege zisizo na rubani na (kushambuliwa) kulengwa kwa Meli ya kubeba ndege za kivita ya Marekani na idadi ya meli za kijeshi za nchi hii.
Katika taarifa hiyo, Jeshi la Yemen kwa mara nyingine tena limesisitiza juu ya kuzuia kupitishwa kwa meli za Israel (katika bahari nyekundu) na kuiunga mkono Ghaza hadi pale vita vitakaposimama na mzingiro wa utawala wa Kizayuni dhidi ya ukanda huu utakapoondolewa.
Imeelezwa katika kauli hii: Kuongezeka kwa safari za ndege za kivita na kufanya mashambulizi zaidi hakutawazuia wananchi wa Yemen kutekeleza wajibu wao wa kidini na kimaadili kwa Taifa Madhulumu la Palestina.
Kabla ya hapo, vyanzo vya lugha ya Kiebrania vilitangaza uanzishwaji wa upigaji wa ving'ora vya onyo katika maeneo (ya Palestina) yanayokaliwa kwa mabavu kufuatia shambulio la kombora la Yemen.
Your Comment