21 Machi 2025 - 02:44
Imani na matendo mema ni funguo za furaha ya Mwanadamu kwa mtazamo wa Qur'an

Hojjat-ul-Islam Madani, katika hafla ya kuhuisha usiku wa 19 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huko Mahdiyeh, Rasht, alisisitiza juu ya umuhimu wa kufikiri kabla ya dhikri katika Usiku wa Lailatul - Qadri, na kuanzisha mambo kama vile imani kwa Mwenyezi Mungu na matendo ya haki kama nguzo mbili za msingi za furaha na ustawi wa Binadamu kwa mtazamo wa Qur'an Tukufu

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul - Bayt (a.s) - ABNA -; Hojjat-ul-Islam, Muhammad Madani alisema siku ya Alhamisi asubuhi, Machi 30, 1403, wakati wa hafla za uhuishaji wa Usiku wa 19 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, uliofanyika Mahdiyeh, Rasht, ambapo aliashiria juu ya umuhimu wa Usiku wa Lailatul - Qadrn akisema: Usiku wa Lailatul - Qadr ni fursa adhimu kwa watu wa fikra na dhikri, kwa sababu dhikri haifikii ukamilifu wake bila ya kufikiri, na mtu ananufaika na dhikri yake kwa njia ya kufikiri.

Akisisitiza furaha na ustawi kuwa ni masuala mawili ya msingi katika maisha ya Mwanadamu, alisema: Ifahamike kuwa ni nini ufunguo wa furaha katika ulimwengu zote mbili. Baadhi ya watu wanaona utajiri na pesa kuwa sababu ya furaha, ambayo ni moja ya mambo yanayoathiri furaha, lakini sio sababu kuu (ya furaha).

Mtaalamu huyu wa masuala ya kidini alifafanua: Uislamu hauna kipingamizi cha kupata pesa kwa njia za halali, ili mradi tu mwenye pesa hizo ni mtoa sadaka na mkarimu. Kwa hivyo, mali na utajiri pekee havitakuwa sababu kuu ya furaha ya Mwanadamu na (havitakuwa na) mwisho mzuri.

Hojjat-ul-Islam Madani aliongeza zaidi: Wengine wanaona kufuata sheria kama moja ya mambo ya furaha ya Mwanadamu. Vile vile uzingatiaji wa sheria ni muhimu katika nchi yoyote, lakini leo sheria nyingi ambazo ni matokeo ya fikra za Binadamu hazifuatwi na hata wabunge (watunga sheria) wanazikiuka.

Akitaja Sayansi na Maarifa kuwa ni sababu nyingine ya Furaha ya Mwanadamu, alisema: Sheria inaweza tu kuwa sababu ya msingi wa Furaha ya Mwanadamu ikiwa itadhibitiwa kwa mujibu wa maumbile ya Mwanadamu na kutekelezwa kwa usahihi kwa siri na kwa uwazi (dhahiri). Kwa hiyo, Sayansi (Elimu) ina nafasi ya juu sana katika Uislamu, ambapo haijapewi umuhimu kama huo katika Dini nyinginezo.

Msemaji wa hafla za Nyusiku za Lailatul- Qadr katika Mahdiyeh ya Rasht amesisitiza kuwa: Katika Dini ya Kiislamu, Sayansi na Wanazuoni wana nafasi maalum na kuna Hadithi nyingi katika uwanja (muktadha) huu, lakini katika historia kumekuwa na Wanachuoni wengi ambao walisimama mbele (dhidi) ya Mwenyezi Mungu na watu, na wakapotezwa.

Akitaja mifano ya mikengeuko iliyosababishwa na upatikanaji (uchumaji) wa Sayansi (elimu), Hojjat-ul-Islam Madani alisema: Silaha wanazotumia makafiri leo hii dhidi ya Wadhulumiwa wa Ulimwenguni, ni matokeo ya miaka mingi ya kujipatia (sayansi) elimu na uzoefu kwa ajili ya kuua, na mashirika yanayojiita ya Haki za Binadamu hayathubutu kukabiliana nao, na wanaishia kujitafutia riziki chini ya kivuli cha watu hao (makafiri na madhalimu).

Akirejelea mambo yanayoathiri Furaha ya Mwanadamu, alisema: Uwezo wa kuwepo kwa Mwanadamu ni mojawapo ya mambo yenye ufanisi katika kufikia furaha. Kwa hiyo, kufaidika na uwezo wa kuwepo (kwa Mwanadamu) ni lazima kuambatane na Ucha-Mungu, kushikamana na amri na hukumu za Mwenyezi Mungu, na kutawala kwa misingi ya haki ili kuleta thawabu maradufu.

Mwishoni, mtaalamu huyo wa masuala ya kidini alisisitiza kuwa: Kwa mujibu wa Qur’an Tukufu, imani kwa Mwenyezi Mungu na matendo mema yanayothibitisha imani hii ni mambo mawili muhimu na ya kimsingi katika mwelekeo wa furaha na ustawi wa Mwanadamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha