Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (A.S.) - Abna -: Wosia wa Hadhrat Ali (amani iwe juu yake), ni moja ya maandiko muhimu ya Kiislamu yaliyo sheheni mafunzo ya maadili, kijamii na kisiasa, na sio tu kwa ajili ya watoto na masahaba (wake), bali pia ni nuru kwa watu wote wanaotafuta ukweli (uhakika) na uadilifu.
Katika wosia huu, kwa kuwa Uadilifu unang'aa kama jua linalowaka, Imam Ali (a.s) anasema ndani yake: “Watendeeni uadilifu maadui zenu, kwa sababu uadilifu ndio msingi ambao ardhi na mbingu zimekaa juu yake. Imam Ali (a.s) anaiona haki (uadilifu) kuwa ni jambo la lazima katika nyanja zote za maisha. Swala nayo ina nafasi ya juu katika maneno yake (a.s) ambapo anasema: "Shikeni Swala, ambayo ni nguzo ya Dini, na huipeleka - huinyanyua - roho juu."
Hadhrat Ali (a.s.) anazichukulia haki za watu, hususan Mayatima na Masikini, kuwa ni Amana ya Mwenyezi Mungu, na anasema: “Linda haki za watu". Pia anasisitiza kutenda wema kwa watu na kuamiliana nao kwa tabia njema, anasema: "Watendee watu vizuri na epuka vurugu." Pia, anaulingania Umma wa Kiislamu kwenye 'Umoja na anachukulia mgawanyiko na mfarakano' kuwa ndio sababu ya uharibifu.
Ali (a.s) anaona 'kuamrisha mema na kukataza maovu' kuwa ni wajibu wa kila Muislamu, na mwishowe, anaielezea subira kuwa ni ufunguo wa wokovu, anasema: “Kuweni na subira katika mambo magumu". Wosia huu ni mwongozo wa milele kwa maisha ya mtu binafsi na ya kijamii.
Wasifu - Sira - wa Imam Ali (amani iwe juu yake), Al-Mortaza al-A'mili.
Your Comment