Mtume (s.a.w.w) ametuelekeza akisema: "Fungeni kwa kuonekana (kwa kuuona) Mwezi, na Fungueni kwa Kuonekana Mwezi". Hivyo tunatarajia kuonekana kwa Mwezi itakuwa ni tarehe 30 au 31".
Dua ya kabla ya alfajiri ikiwa kama dua maarufu zaidi ya kabla ya asubuhi kuingia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani imepokelewa kutoka kwa Imam Baqir (AS). Uhusiano kati ya dhana ya juu ya Dua hii na nafasi ya Uimamu ni moja ya mada muhimu katika maelezo ya Dua hii.
Wosia wa Hadhrat Ali (amani iwe juu yake), ni moja ya maandiko muhimu ya Kiislamu yaliyosheheni mafunzo ya kimaadili (kiakhlaq), kijamii na kisiasa, na sio tu kwa ajili ya watoto na masahaba zake, bali pia ni nuru kwa watu wote wanaotafuta ukweli (uhakika) na uadilifu.