29 Aprili 2025 - 16:50
Matendo Mema katika Dua na Swala za Sunna (Sehemu ya 1)

Huu ni mkusanyiko uliokusanya baadhi ya matendo ya kufanya usiku na mchana, swala za Sunnah zilizopokewa, ponyo, kinga, dhikir, dua za ajabu, athari za baadhi ya Aya na ufupisho wa kuwafanyia adabu waliokufa, nimezikusanya ili niziambatanishe kwenye Mafatihul Jinani kisha kitabu kikamilike kwa njia zote na iwe na manufaa kwayo yaliyotimia.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Katika makala hii murwa tunakuletea andiko muhimu kuhusiana na "Matendo Mema katika Dua na Swala za Sunna (Sehemu ya 1)". Ni makala maridadi iliyosheheni faida za kielimu na maarifa kutoka Mwandishi Mahiri na Mhudumu wa Madrasat Ahlul-Bayt (a.s), ndugu yetu katika Imani, Sheikh Hassani Juma Bussi (Mwenyezi Mungu azidi kumhifadhi katika kuhudumia Uislamu na Waislamu).

وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِنْدَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا 

UTANGILIZI WA MTUNZI 

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye huongoza mbinguni na akafanya Ibada za Sunnah kwenye Dua,  na Rehema na Amani ziwe juu ya yule uliyemtanguliza katika kumteua Muhammad (s.a.w.w) akiwa ni Nabii wa Mwisho wa Manabi (a.s), na juu ya Kizazi chake kitoharifu (a.s), ambacho ni taa zenye kuwaka na kuangazia watu,  khususan Al-Imam Al-Mahdi (a.s), ambaye ni wa mwisho wa Mawasii (amani iwe juu yao).

Na baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu na kumtakia Rehema Mtume wake (saww) na kizazi chake kitoharifu: Mwenye Madhambi ambaye ameuchafua uso wake kwa Madhambi, mwenye mapungufu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Abbas Ibn Muhammad Ridha Al-Qummiy Mwenyezi Mungu (amuwie radhi) anasema: 

Huu ni mkusanyiko uliokusanya baadhi ya matendo ya kufanya usiku na mchana, swala za Sunnah zilizopokewa, ponyo, kinga, dhikir, dua za ajabu, athari za baadhi ya Aya na ufupisho wa kuwafanyia adabu waliokufa, nimezikusanya ili niziambatanishe kwenye Mafatihul Jinani kisha kitabu kikamilike kwa njia zote na iwe na manufaa kwayo yaliyotimia.

Na nimekiita Matendo mema yabakiayo katika Dua na Swala za Sunnah. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:


وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِنْدَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا


"Na matendo mema yabakiayo ndiyo bora mbele ya Mola wako kwa malipo na tumaini bora". Surah Al-Kahf (18 : Aya ya 46).

Na nimekipanga kitabu hiki katika milango sita, na pia mwisho wake:

Mlango wa kwanza: Tutasoma katika sehemu ya matendo ya usiku na mchana.

Mlango wa pili: Tutasoma baadhi ya Swala za Sunnah.

Mlango wa tatu: Tutasoma: Ponyo la maumivu,  maradhi, ugonjwa wa viungo, homa na mengineyo.

Mlango wa nne: Tutasoma Dua zilizochaguliwa kutoka kitabu cha Al-Kafiy.

Mlango wa tano: Tutasoma baadhi ya kinga na Dua za Kustaajabisha zilizodonolewa kutoka kitabu cha Mahjud Dawaat Wal-Mujitanaa.

Mlango wa sita: Tutasoma athari za baadhi ya sura na Aya, na kutaja mambo tofauti tofauti.

Mwisho: Tutasoma ifupisho wa hukumu za maiti.

 Na tumaini la ujasiri na uaminifu kwa ndugu zangu waaminifu wa Shi'ah wa Amirul Muuminina Ally as, wasinisahau wakati wa kuomba dua na kuomba msamaha, na ile hali Mimi ni mfanya ma'asi katika maisha na baada ya kufa.

Abbasi Bin Muhammad Alqummiy.

UTANGILIZI WA MTARJUMI

بسم الله الرحمن الرحيم 
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma mwenye kurehemu

Kila sifa njema ni za Mola wa Ulimwengu. Na Rehema na amani ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad saww na juu ya Kizazi chake ambacho Mwenyezi Mungu amekilinda na uchafu na kukitakasa kabisa.

Ama baada ya hayo; Hii ni ni tafsiri ya kitabu kiitwacho: Na matendo mema yabakiayo.
Sababu iliyonipelekea kutoa juhudi hii ni mambo mawili:-

Kwanza: Ni ili iwe ni uthibitisho wa mapenzi yangu kwa Mtukufu Mtume Muhammad saww, ambaye kwa kumpenda yeye (Mtume saww) matendo mema yanakubaliwa, na kwa kumpenda yeye (Mtume saww) twaa inafaa kwa kupanda mpaka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na ili iwe ni uthibitisho wa mapenzi yangu kwa Amirul Muuminina Ally bin Abi Twalib as ambaye kwa kumpenda yeye (Ally) matendo mema yanakubaliwa, na kwa kumpenda yeye (Ally) twaa inafaa kwa kupanda mpaka kwa Mtukufu Mtume saww Mtukufu.

Pili: Ni ili taa na Nuru kwa aliyetenga wakati wake kwa ajili ya kusoma kitabu hiki  au kutega sikio, na yeye ni Shahidi, miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewasifu ndani ya Qur-an tukufu kuwa ni waja wake, na akawabashiria hilo pale aliposema: 

وأنابوا إلى الله لهم البشرى، فبشر عباد (١٧) الذين يستمعون القول فيتبعون احسنه أولئك الذين هداهم الله أولئك هم أولوا الألباب (١٨)ز


...Na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata biashara njema. Basi wape habari njema waja wangu. Ambao husikiliza (husoma) maneno (mengi yanayosemwa) kisha wakafuata mazuri yake zaidi. Hao ndiyo aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndiyo wenye akili."39:17-18. Zumar.

Imeandikwa na: Sheikh Hassani Juma Bussi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha