29 Machi 2025 - 21:36
Eid Al_Fitri yatangazwa Tanzania kabla ya kuonekana kwa Mwezi

Mtume (s.a.w.w) ametuelekeza akisema: "Fungeni kwa kuonekana (kwa kuuona) Mwezi, na Fungueni kwa Kuonekana Mwezi". Hivyo tunatarajia kuonekana kwa Mwezi itakuwa ni tarehe 30 au 31".

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -; Eid Al_Fitri yatangazwa Tanzania kabla ya kuonekana kwa Mwezi. Sheikh wa Mkoa wa Dar-es-salaam - Tanzania, ametangaza kwa niaba ya Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt.Abubakar Zubair bin Ali, kuwa Sala ya Eid Al_Fitri itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme wa 6 wa Morocco, uliopo Kinondoni - Jijini Dar-es-salaam, Tanzania.

Baada ya Sala ya Eid, mida ya jioni, litafanyika Baraza la Eid katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar-es-salaam, ambapo yatazungumzwa masuala mbalimbali juu ya Maendeleo na Ustawi wa Uislamu nchini Tanzania.

Mgeni Rasmi katika Baraza hili la Eid atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Eid Al_Fitri yatangazwa Tanzania kabla ya kuonekana kwa Mwezi

Sheikh wa Mkoa wa Dar-es-salaam, Sheikh Walid Alhad Omar kuhusu ni lini Siku ya Eid itakuwa, amesema:

Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) ametuelekeza akisema: "Fungeni kwa kuonekana (kwa kuuona) Mwezi, na Fungueni kwa Kuonekana (kwa kuuona) Mwezi".

Hivyo  tunatarajia kuonekana kwa Mwezi itakuwa ni tarehe 30 au 31. Hivyo Eid inatarajiwa kuwa tarehe 31 Machi, 2025 au tarehe 1 April, 2025.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha