Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (AS) - Abna -; Matukio ya hivi majuzi nchini Syria na kutawaliwa na makundi ya kigaidi nchini humo yametoa fursa nyingine kwa uchokozi wa utawala ghasibu wa Kizayuni, pamoja na kuimarisha udhibiti wake katika maeneo kama vile Miinuko ya Golan, kuyakalia maeneo mengine yanayopakana na Syria na kushambulia maeneo kadhaa ya nchi hiyo.
Lakini katika wakati huo huo, mbali na vikosi vya jeshi la Kizayuni, vyombo vya habari vinavyouunga mkono utawala huu pia vina nafasi kubwa katika kuleta utulivu na kuimarisha ukaliaji wa mabavu wa utawala huu.
Katika makala iliyogusia nafasi iliyochukuliwa na vyombo hivyo vya habari katika uvamizi wa jeshi la Kizayuni, tovuti ya Model East Eye iliandika: Tangu kukaliwa kwa mabavu Miinuko ya Golan ya Syria mwaka 1967, utawala wa Kizayuni umeuchukulia Mlima Hermon kuwa ni ngome kubwa na muhimu ya kiistratijia.
Kwa mtazamo wa utawala wa Kizayuni, Miinuko ya Golan inachukuliwa kuwa muhimu sio tu kwa usalama wa taifa, bali pia kwa maendeleo na usambazaji wa rasilimali za maji. Aidha, Milima ya Golan daima imekuwa ikizingatiwa kama turufu katika mazungumzo yoyote ya amani na Syria.
Katika miongo kadhaa baada ya kukaliwa kwa mabavu, siasa za utawala wa Kizayuni zilibadilika-badilika kati ya nia ya kufanya mazungumzo na nia ya kuhifadhi Miinuko ya Golan. Katika nyakati tofauti, baadhi ya mawaziri wakuu wa utawala wa Kizayuni (katika miongo kadhaa iliyopita) walikubali mipango ya kujiondoa ili kubadilishana amani na kuhalalisha uhusiano wa kidiplomasia, lakini kwa bahati mbaya ukaliaji wa eneo hili unaendelea.
Baada ya kuporomoka kwa utawala wa Bashar al-Assad, utawala wa Kizayuni ulipanua maendeleo yake na kuteka maeneo zaidi ya Syria. Mojawapo ya shabaha kuu za maendeleo haya daima imekuwa Mlima Hermon, wenye urefu wa kimkakati ambao una nafasi maalum katika milingano ya kijeshi ya eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa Mwezi Disemba utawala wa Kizayuni uliteka kilele cha juu kabisa cha Syria ambacho kiko zaidi ya mita 2,800 kutoka usawa wa bahari; Kwa hakika, hatua hii inaonyesha kuendelea kwa sera ya uvamizi nchini Syria.
Vyombo vya habari vingi vya Israeli vimekuwa na mijadala na mabishano mengi kuhusu masharti wanayopaswa kutumia kuelezea "mafanikio" haya mapya, na hii inaonyesha nia ya wazi ya kuujumuisha Mlima Hermon kwenye maeneo yanayokaliwa kimabavu.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Kizayuni kwa mara ya kwanza vilikuwa vikilitaja eneo hilo kwa anuani ya "Hermon ya Syria", lakini baadaye waligundua makosa yao. Pole pole, kwa kuelewa kwamba maneno yanayoendana na malengo ya kikoloni ya utawala wa Kizayuni yanapaswa kutumika; Katika suala hili, mapendekezo mapya (ya kuliita kwa jina jipya eneo hilo) yalitolewa, ikiwa ni pamoja na "Taji Hermon", jina ambalo linahusu shairi lililoandikwa na mmoja wa viongozi na takwimu maarufu za Zionism (Uzayuni), Ze'ev Zabotinsky, katika karne iliyopita.
Madhumuni ya hatua hii ni dhahiri kuutenganisha Mlima Hermon na utambulisho wake wa Syria na kuthibitisha utawala wa Uzayuni juu ya Muinuko huu wa kimkakati.
(Mizinga ya Israeli kwenye Mlima Hermoni wa Syria mnamo mwaka 1974).
Ukoloni na Kujitanua
Si vyombo vya habari pekee vinavyotumia msamiati na mbinu hii. Kwa upande mmoja, mashirika ya watalii pia huuza tiketi ili kupanda "kilele cha juu zaidi katika Israeli"; Kwa upande mwingine, uvamizi wa maeneo mapya unaofanywa na jeshi la kigaidi la utawala huu unakabiliwa na majibu chanya na kukaribishwa na Serikali bandia ya utawala huo. Njia hii inafanywa bila kuwa na wasiwasi juu ya matokeo ya hatua zilizotajwa na kuzingatia hatima ya watu wa eneo hilo na nchi jirani.
Inafaa kukumbuka kuwa uhalali wa kisheria wa serikali ya kizayuni kukalia kimabavu eneo hili haukubaliki kwa njia yoyote. Kwa sababu hadi sasa eneo hili halijakuwa tishio kwa asili yake na hoja ya (kuchukua) hatua ya kuzuia kuukalia Mlima Hermon haikubaliki kwa hali yoyote ile. Baadhi ya matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa utawala huo haramwa kizayuni na Waziri Mkuu wake yanaakisi azma ya utawala wa Kizayuni ya kukalia kwa mabavu eneo hili kwa namna ya kudumu.
Ukimya wa Serikali ya mpito ya Syria kuhusiana na mashambulizi ya utawala huo, huku baadhi ya serikali za mikoa zikilaani vitendo vya utawala huo. Hatimaye amani na uthabiti wa eneo hilo umefungamana na uthabiti wa Syria, na kwa hivyo jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za haraka dhidi ya hatua haramu za utawala wa Kizayuni.
Your Comment