“Tuko tayari kuwapokea waathiriwa walioumia,” amesema Prabowo siku ya Jumatano kabla ya kuelekea katika ziara yake ya Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), ambapo atazitembelea Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Uturuki, Misri, Qatar na Jordan.
“Tuko tayari kupeleka ndege kuwachukua. Tunakadiria idadi ya awali kuwa ni takriban watu 1,000 katika awamu ya kwanza,” aliongeza.
Alibainisha kuwa Wapalestina walioumia pamoja na “watoto waliopitia mishtuko mikubwa ya kiakili na waliopoteza wazazi wao” watapewa kipaumbele.
Amesema amemuelekeza waziri wake wa mambo ya nje kufanya mazungumzo na viongozi wa Palestina pamoja na “pande husika katika eneo hilo” kuhusu jinsi ya kuwaondoa na kuwaokoa Wapalestina walioumia au yatima kutoka Gaza.
Waathiriwa hao watakaa Indonesia kwa muda tu hadi watakapopona na hali kuwa salama kwao kurejea makwao.
Indonesia, taifa lenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani, imekuwa ikitoa wito kwa muda mrefu wa kusitishwa kwa vita vya kinyama vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.
342/
Your Comment