10 Aprili 2025 - 16:21
Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria yalaani Serikali kwa mauaji ya Waandamanaji 26 wanaounga mkono Palestina, na kuwaweka kizuizini 274

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, matukio kadhaa ya amani ya kidini yaliyoandaliwa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria chini ya uongozi wa Sheikh Zakzaky, likiwemo Kongamano la Mwaka la Mauaji ya Zaria ya mwaka 2015 na programu ya Nisfu / Nusu Sha’ban kwa ajili ya kuadhimisha Maulid ya Imam Mahdi (a.t.f.s), yaliripotiwa kuvurugwa na vikosi vya usalama.

Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) - ABNA -: Kwa mujibu wa taarifa hiyo, matukio kadhaa ya amani ya kidini yaliyoandaliwa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria chini ya uongozi wa Sheikh Zakzaky, likiwemo Kongamano la Mwaka la Mauaji ya Zaria ya mwaka 2015 na programu ya Nisfu / Nusu Sha’ban kwa ajili ya kuadhimisha Maulid ya Imam Mahdi (a.t.f.s), yaliripotiwa kuvurugwa na vikosi vya usalama.

Harakati ya Kusini Magharibi mwa Nigeria imelaani vikali utawala wa Rais Bola Ahmed Tinubu kuhusiana na mauaji ya waandamanaji 26 wanaoiunga mkono Palestina na kuendelea kuzuiliwa watu wengine 274 wakiwemo watoto wadogo na wagonjwa mahututi wakati wa maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka 2025 mjini Abuja.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mnamo Jumanne, Aprili 9, 2025, Miftahu Zakariya, Mratibu wa Kusini Magharibi wa Harakati ya Kiislamu, alishutumu maajenti wa usalama chini ya utawala wa Tinubu kwa kuanzisha mashambulizi dhidi ya waandamanaji wa amani wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria (IMN), inayoongozwa na Ibraheem Zakzaky.

"Tunalaani kukatizwa kwa shughuli za Kiislamu na kuwatesa wafuasi wa vuguvugu la Kiislamu huko Abuja," Zakariya alisema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, matukio kadhaa ya amani ya kidini yaliyoandaliwa na kundi hilo, yakiwemo Mkutano wa Mwaka wa Mauaji ya Zaria 2015 na programu ya Nisfu / Nusu Sha’aban kwa ajili ya kuadhimisha Maulid ya Imam Mahd i(a.t.f.s), yaliripotiwa kuvurugwa na vikosi vya usalama.

Lakini ukandamizaji wa kikatili wa maandamano ya Siku ya Quds ulileta shutuma kali zaidi.

"Maajenti wa usalama, haswa Kikosi cha Walinzi, walishambulia waandamanaji kwa amani Siku ya Kimataifa ya Quds ya 2025 huko Abuja, siku ambayo iliadhimishwa katika Msikiti wa Usman Bin Affan kando ya Aminu Kano Crescent, Abuja, Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani, 28 Machi 2025. Wakati wa shambulio hilo, Jeshi liliua waandamanaji 26 na kuwakamata 274, wakiwemo watoto 60," Zakariya alifichua.

Aidha alidai kuwa watu 11 kati ya waliokamatwa ni wagonjwa mahututi na bado wapo kizuizini.

"Hadi wakati huu, polisi walikataa kuwaachilia waandamanaji waliozuiliwa na maiti za wale waliouawa na Jeshi," aliongeza.

Zakariya pia alitaja ripoti zinazoonyesha mpango wa usalama wa siri wa kuvamia jamii ambazo ni wafuasi wa vuguvugu la Kiislamu kule wanakoishi katika maeneo nyumba zao.

"Ripoti za vyombo vya habari zilifichua mpango wa mawakala wa usalama kushambulia maeneo na jamii ambapo wafuasi wa vuguvugu la Kiislamu wanaishi," alisema.

Cha kusikitisha ni kwamba kundi hilo pia lilithibitisha kifo cha muandamanaji aliyezuiliwa chini ya hali ya kutiliwa shaka. "Majina ya walioaga dunia hivi majuzi ni pamoja na Shaheed Huzaifa Muhammad, kutoka Tudun Iya, Jimbo la Katsina, ambaye aliuawa shahidi Jumatatu, Aprili 7, 2025, karibu saa kumi na mbili jioni katika Machinjio ya SARS, Guzape, Abuja," Zakariya alisema.

Jumuiya hiyo imesisitiza kuwa, shughuli zao za kila mwaka za Siku ya Quds, sehemu ya maonyesho ya kimataifa ya mshikamano na wananchi wa Palestina yaliyoanzishwa mwaka 1979 na Kiongozi wa Iran Ayatollah Khomeini (RA), yalifanyika kwa amani katika majimbo 17 ya Nigeria, yakiwemo Lagos, Kano na Sokoto, bila ya tukio lolote (la uvunjifu wa amani).

"Kuwa Muislamu au mfuasi wa watu wa Palestina kamwe hakuwezi kuwa uhalifu ndani ya Nigeria na duniani kote," Zakariya alisema.

"Kwa hakika, kabla ya sasa jumuiya ya kimataifa ilikuwa na ufahamu kamili kwamba utawala wa Bola Ahmed Tinubu ni muungaji mkono na mtoa sapoti kwa Palestina."

Alirejelea kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Maitama Tuggar, ambaye, alipokuwa akizungumza na Al Jazeera Machi 2025, aliripotiwa kusema: "Israel lazima ikomeshe vita vyake dhidi ya Gaza, na ulimwengu unahitaji kuacha msimamo wake wa ndumakuwili kuelekea mauaji ya yanayofanyika katika eneo lililozingirwa (la Ukanda wa Gaza)."

Hapo awali IMN ilishutumu vikosi vya usalama vya Nigeria kwa kukataa kuachilia maiti 26 za wanachama wake waliouawa wakati wa maandamano ya kuunga mkono Palestina huko Abuja.

Vuguvugu hilo maarufu pia lilishutumu Polisi kwa kuwaweka kizuizini wanachama 274 waliokamatwa wakati wa maandamano yao ya hivi majuzi, wakiwemo watoto 60 na wagonjwa 11 ambao ni mahututi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha