Ismail Baghaei, ameandika hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X ikiwa ni kuonesha hisia zake kuhusu mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza na kugusia ripoti ya msemaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF) huko Palestina na kusema kuwa ripoti hiyo imekuwa ikitolewa takriban kila siku kwa karibu miaka miwili sasa.
Amesema: "Msemaji wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) huko Palestina anasema kuwa: Idadi ya watoto wanaouawa tangu kuanza vita vya Ghaza imefikia wastani wa watoto 27 kwa siku, na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekuwa likilaani mara kwa mara jinai za Israel.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetangaza rasmi kwamba jinai za utawala ghasibu wa Israel ni mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina. Nayo Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imetoa amri za kusakwa na kutiwa mbaroni viongozi wa Israel; lakini bado mauaji yanaendelea.
Vile vile amesema kuwa, watoto wengi zaidi wanakufa kila siku huko Ghaza imma kwa mashambulizi ya mabomu au kutokana na siasa za makusudi za utawala ghasibu wa Israel za kuwaua kwa njaa raia hao; na hizo ni jinai za wazi kabisa za kivita.
342/
Your Comment