19 Aprili 2025 - 20:46
Source: Parstoday
Mwito wa Iran kwa jamii ya kimataifa wa kuzingatiwa hali ya Gaza

Esmail Baghaei, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia kwa uzito jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.

Baghaei ameandika kwenye akaunti yake ya X: "Kila siku, watoto wengi zaidi wanakufa katika mashambulizi ya mabomu huko Gaza au kutokana na sera za makusudi za utawala wa Kizayuni za kuwaua kwa njaa raia." Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, vitendo hivi vinachukuliwa kuwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na mauaji ya halaiki.

Katika radiamali yake ya kuendelea mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Gaza sambamba na kuashiria ripoti ya msemaji wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) huko Palestina, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameandika: "Ripoti hii haihusu Enzi za Kati, wala haihusu Enzi za Giza; maafa haya yamekuwa yakijirudia kila uchao kwa takriban miaka miwili.

Abu Khalaf, msemaji wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) huko Palestina ameripoti kuwa, idadi ya watoto waliouawa tangu kuanza kwa vita vya Gaza imefikia wastani wa watoto 27 kwa siku.

Msemaji huyo wa UNICEF ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kushinikiza kibali cha kuruhusu misaada kuingia Gaza, akisisitiza kuwa: "Kuingia kwa misaada Gaza hakupaswi kutumiwa kama wenzo wa muamala au kutaka punguzo." Akiendelea kutoa takwimu za hivi punde za vita vya Gaza, msemaji huyo wa UNICEF amesema kuwa kuna watoto yatima 39,000 huko Gaza.

Hii ni katika hali ambayo, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limelaani mara chungu nzima jinai za utawala wa Kizayuni;  Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imezitaja jinai za utawala ghasibu wa Israel kuwa ni mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina; na imetoa hati za kukamatwa kwa viongozi wa utawala huo wa kihalifu na haramu; lakini mauaji ya halaiki ya Wapalestina yangali yanaendelea.

Mwito wa Iran kwa jamii ya kimataifa wa kuzingatiwa hali ya Gaza

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuzingatia imani na misingi yake katika kuwaunga mkono wanyonge, daima imekuwa muungaji mkono mkuu wa wananchi wa Palestina katika miaka ya hivi karibuni. Baada ya Operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqswa, Iran pia imesisitiza kwa uzito suala la kushughulikia jinai za utawala wa Kizayuni katika mikutano ya kieneo na nchi jirani na katika majukwaa ya Umoja wa Mataifa.

Wapalestina ndio watu wanaodhulumiwa zaidi duniani, huku wakikabiliwa na jinai zisizo na mithili za Wazayuni katika kipindi cha miongo minane iliyopita. Wazayuni sio tu kwamba wameikalia kwa mabavu jiografia ya Palestina kwa uungaji mkono wa Wamagharibi, bali pia wanafanya ghasia zisizo na kifani dhidi ya Wapalestina kwa uungaji mkono wa Wamagharibi hususan Marekani na mfano wa wazi ni mauaji ya kimbari huko Gaza.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia inaunga mkono harakati za muqawama za kupigania ukombozi  za Waapalestina ambazo ni za kupigiwa. Muqawama wa Palestina una mizizi katika mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa ni muungaji mkono wa nchi na mataifa ya Kiislamu inaona kuwa ni wajibu wake kuunga mkono kadhia ya watu wa Palestina.

Mwito wa Iran kwa jamii ya kimataifa wa kuzingatiwa hali ya Gaza

Kwa kutilia maanani jinai za Wazayuni huko Gaza na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na wavamizi kwa mabavu, ni jambo la lazima kuchukuliwa hatua ili kukabiliana na mwenendo huo kwa kuweko mshikamano na ushirikiano baina ya ulimwengu wa Kiislamu.  Iran ikiwa nchi iliyoko mstari wa mbele katika kuunga mkono watu wa eneo hili, itakuwa na nafasi ya kimsingi na yenye ufanisi katika kuleta ushirikiano na fikra za pamoja za kuunga mkono kadhia ya Palestina.

Kukomesha uvamizi huo, kukabiliana na njama za pamoja za Wamarekani na Wazayuni, kuelezea mchakato usio na natija na kutwisha mwenenedo wa mapatano, na kutilia maanani sana mauaji ya halaiki ya Wazayuni ni miongoni mwa masuala muhimu ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakuwa na nafasi yenye taathira katika eneo, na fikra za waliowengi katika Ulimwengu wa Kiislamu pia yanaunga mkono hatua hizo.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha