20 Aprili 2025 - 00:07
Hawzat Imam Ali (a.s) chini ya Bilal Muslim Tanga, Kitengo cha uhamasishaji ilifanya Ziara ya uhamasishaji kwa Waumini wa Bilal Muslim Mwembeni -Tanga

Lengo la ziara hii, kuhamasishana na kuelezea umuhimu wa kutoa Sadaka hasa katika kuichangia Masira ya Imam Hussein (a.s).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Hawzat Imam Ali (a.s) iliyopo chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanga, Tanzania - Kitengo cha uhamasishaji wa Michango ya uwezeshaji wa masira ya Imam Hussein (a.s) - Siku ya Ijumaa tarehe 18/04/2024 kilifanya ziara muhimu na kukutana na Waumini wa Bilal Muslim Mwembeni.

Lengo la ziara hii, kuhamasishana na kuelezea umuhimu wa kutoa Sadaka hasa katika kuichangia Masira ya Imam Hussein (a.s).

Katika ziara hii, Samahat Sheikh Swaleh Abdur-Rahman amewaeleza Waumini fadhila za kutoa Sadaka na ubora wake.

Kitengo cha uhamasishaji kitaendelea na ziara hizi mpaka Mwezi wa Muharram Insha'Allah.

Waliofanikisha Ziara hii: Sheikh Swaleh na Sheikh Murshid Tibaijuka.

Imeripotiwa na:
Kitengo cha Ripoti  za Tabligh. Hawzat Imam Ali (a.s) - Pangani.

Your Comment

You are replying to: .
captcha