Akigusia uhusiano wa kihistoria, kiutamaduni na kifamilia kati ya mataifa ya Iran na Azerbaijan, Rais Pezeshkian ameongeza kuwa: "Mafungamano hayo yatatayarisha njia ya kuundwa njia mwafaka kwa ajili ya kupanua ushirikiano wa kieneo."
Daktari Pezshekian amesema hayo mjini Baku katika kikao cha wajumbe wa ngazi za juu kutoka Iran na Jamhuri ya Azerbaijan na kueleza kufurahishwa kwake na kuwepo mjini humo na kusema: "Ni heshima kubwa kuwepo katika Jamhuri ya Azerbaijan na kushiriki katika mkusanyiko wa maafisa kutoka nchi yenye ndugu na rafiki." Natumai kuwa safari hii na makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mikutano ya awali ya wataalamu itakuwa mwanzo wa hatua kubwa zaidi kuelekea kukuza uhusiano kati ya nchi hizi mbili.
Kadhalika amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikisisitizia kuunga mkono haki za watu wa Azerbaijan na inaamini kuwa eneo la Karabakh ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya ardhi ya Jamhuri ya Azerbaijan.
Rais Pezeshkian ameutaja uwepo wa ujumbe wa Iran mjini Baku kuwa ni ishara ya azma kubwa ya nchi hizo mbili ya kuimarisha uhusiano, kuimarisha umoja na kupanua mshikamano kati ya pande mbili hizo.
Kwa upande wake, Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan akimkaribisha Rais wa Iran, alisema katika mkutano huo: "Safari hii ni muhimu sana." Katika mkutano huu, tumejadili masuala mengi na kusisitiza maendeleo ya mahusiano ambayo yanatumikia maslahi ya nchi zote mbili.
Mkutano huo unafuatia mwelekeo mpana zaidi katika kanda ambapo nchi zinataka kurekebisha uhusiano uliodorora na kujenga ushirikiano mpya wa kiuchumi na kimkakati. Safari ya Pezeshkian nchini Azerbaijan inasisitiza umakini wa Tehran katika kuleta utulivu wa eneo lake jirani.
342/
Your Comment