Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlulbayt (a.s) - ABNA -: Jeshi la Makombora la Jeshi la Silaha la Yemen limetekeleza operesheni ya kijeshi ikilenga Kituo cha Anga cha Nevatim katika eneo la Negev, Kusini mwa Palestina inayokaliwa kimabavu, kwa kutumia kombora la Hipersoniki la Balistiki.
Jeshi la Silaha la Yemen lilitoa taarifa ifuatayo:
"Katika kutoa sapoto na msaada kwa watu wa Palestina wanaodhulumiwa na wapiganaji wao, na kukataa jinai ya mauaji ya kimbari inayofanywa na adui Mzayuni dhidi ya watu wetu katika Ukanda wa Gaza, Jeshi la Makombora la Jeshi la Silaha la Yemen limetekeleza operesheni ya kijeshi ikilenga Kituo cha Anga cha Nevatim katika eneo la Negev, Kusini mwa Palestina inayokaliwa kimabavu kwa kutumia kombora la Hipersoniki la Balistiki.
Operesheni hiyo imefanikiwa kufikia lengo lake, Tunamshukuru Allah kwa hilo.
Jeshi la Silaha la Yemen linafafanua likisema: "Kwa kutegemea msaada wa Allah na kutafuta msaada Wake, tutaendelea kukuza uwezo wetu wa kijeshi ili kukabiliana na maendeleo ya sasa na kuvunja kiburi na majivuno ya mashambulizi ya Marekani".
Wajeshi hawa wa Yemen, wanaendelea kuthibitisha kwamba wataendelea na operesheni zao za kijeshi katika kuwasaidia watu wa Palestina wanaodhulumiwa katika Ukanda wa Gaza, na kwamba operesheni hizi hazitasitishwa hadi uhasama dhidi ya Gaza uishe na vizuizi dhidi yao viondolewe."
Your Comment