Imeelezwa kuwa, migogoro inayoongezeka duniani ndiyo inayochochea ongezeko la matumizi hayo.
Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Masuala ya Amani (SIPRI) yenye makao yake nchini Sweden imesema kuwa, ongezeko la matumizi ya kijeshi limeshuhudiwa zaidi barani Ulaya na eneo la Mashariki ya Kati.
Mtafiti wa Mpango wa Matumizi ya Kijeshi na Uzalishaji wa Silaha katika taasisi ya SIPRI, Xiao Liang, amesema matumizi ya kijeshi yamekuwa yakiongezeka katika nchi zaidi ya 100 duniani hali inayotishia kuchochea mivutano zaidi.
"Ongezeko hili la matumizi ya kijeshi ambalo halijawahi kushuhudiwa, litakuwa na athari kubwa sana kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa sababu ili kufadhili ongezeko hilo kubwa, nchi zitatakiwa kuchukua maamuzi kuhusu bajeti zao," alisema.
Mataifa yote ya Ulaya kasoro Malta yameongeza maradufu matumizi ya kijeshi huku Marekani ikisalia kileleni ambapo matumizi yake ya kijeshi yalifikia dola bilioni 997.
Bajeti ya kijeshi ya nchi mbalimbali duniani imeongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa kutokana na sababu kadhaa kama vile mfumuko wa bei, vita vya Russia dhidi ya Ukraine na jitihada zinazofanywa na Marekani kuipiku China.
Vita vya Russia dhidi ya Ukraine vimezifanya nchi za Ulaya kutazama upya bajeti zao za kijeshi. Nchi mbalimbali aidha zilitangaza bajeti zao mpya za matumizii ya kijeshi tangu kuanza kwa mashambulizi ya awali ya makombora ya Russia dhidi ya miji mbalimbali ya Ukraine Februari 24 mwaka jana.
342/
Your Comment