Kulingana na ripoti ya shirika la habari la Abna, likinukuu Russia Today, Tal Ortan, mtaalam wa masuala ya kijeshi wa utawala wa Kizayuni na afisa wa zamani wa idara ya ujasusi ya kijeshi ya utawala huo, alionya kuwa idara za ujasusi za Tel Aviv zinapaswa kuifuatilia Misri kwa karibu kwani nchi hiyo inajiandaa kwa vita na utawala wa Kizayuni.
Gazeti la Kizayuni la Israel Hayom pia liliripoti kwamba uhusiano kati ya Cairo na Tel Aviv umefikia kiwango chake cha chini kabisa katika ngazi za kisiasa na kwamba mikataba ya amani na kurejesha uhusiano ambayo ilikuwa na matumaini makubwa inafifia.
Vichwa vya habari vya magazeti ya Kiebrania katika siku za hivi karibuni pia vililenga kuimarika kwa nguvu za kijeshi za Misri na utayari wake wa kivita kutokana na kufanyika kwa mazoezi makubwa ya kijeshi na Marekani, Urusi na China.
Your Comment