Gazeti la Ufaransa la Le Figaro limeripoti kwamba wachunguzi waligundua video ambayo mhalifu huyo alijirekodi wakati akitenda uhalifu huo, ambapo anamtukana raia huyo Muislamu na kumtusi Mwenyezi Mungu kwa lugha chafu.
Gazeti hilo limemnukuu Mwendesha Mashtaka wa Umma wa Jamhuri katika eneo la Alice, Abdelkarim Grini, akisema kwamba alikuwa akichunguza "dhana zote, ikiwa ni pamoja na dhana ya hujuma dhidi ya Uislamu."
Muuaji hakujua kuwa kamera za ulinzi za msikiti huo zilikuwa zikimrekodi hadi alipokamilisha uhalifu huo na ndipo alipofoka: "Nitakamatwa, ni hakika!" na kisha akakimbia. Mhalifu huyo alikamatwa muda mfupi baadaye.
Baada ya kuchunguza utambulisho wake, polisi ya Ufaransa imebaini kuwa raia huyo si Muislamu.
Uhalifu huo ulifanyika Ijumaa asubuhi ndani ya msikiti huo. Mwathiriwa, mwenye umri wa kati ya miaka 23 na 24, hakupatikana hadi waumini walipoanza kuwasili msikitini hapo kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.
342/
Your Comment